Azam na Yanga zitakutana na hawa kwenye michuano ya CAF.
Timu
zitakazoiwakilisha Tanznaia kwenye mashindano ya kimataifa kwa ngazi ya
vila hii leo zimefahamu wapinzani wake katika michuano hiyo kwa msimu wa
mwaka 2014 / 2015 baada ya ratiba ya michuano ya Klabu Bingwa barani
Afrika na kombe la shirikisho kupangwa huko Cairo.
Ratiba hiyo
inaonyesha kuwa mabingwa wa Tanzania Azam Fc wamepangwa kucheza na Al
Mereikh kwenye raundi ya kwanza ya ligi ya mbingwa huku wawakilishi toka
Zanzibar KMKM wakicheza na timu nyingine toka Sudan ya Al Hilal .
Azam wataanzia nyumbani dhidi ya Al Merreikh |
Timu nyingine
toka Tanzania Yanga itacheza na timu ya jeshi la ulinzi ya Botswana BDF
huku Polisi ya huko Zanzibar ikicheza na CF Mounana ya nchini Gabon .
Ratiba
inaonyesha kuwa michezo ya kwanza itafanyika kati ya tarehe 13 , 14 na
15 mwezi wa pili mwakani huku mechi za marudiano zikifanyika wiki mbili
baadae yaani tarehe 26 , 27 mwezi wa pili na tarehe 1 mwezi machi .
Azam fc na Yanga zinatarajia kuanzia nyumbani huku KMKM wakianza ugenini huko Omdurman nchini Sudan .
Mchezo kati ya
Azam Fc na Al Merreikh utakuwa maalum kwa beki mpya wa timu hiyo ya
Tanzania Serge Paschal Wawa ambaye atakuwa na nafasi ya kukabiliana na
timu yake ya zamani kwa mara ya kwanza tangu aliposajiliwa toka Al
Mereikh wiki chache zilizopita .