Hatimaye Martini Kadinda Kuoa Soon ili Kumaliza Maneno Maneno Kuwa Hajiwezi

Na Laurent Samatta
MBUNIFU wa mavazi Bongo, Martin Kadinda, amesema kuwa baada ya kuishi bachela kwa miaka mingi amepanga kuoa ‘ soon’ mwanamke ambaye ni mpenzi wake wa siku nyingi ili kumaliza maneno ya watu kuwa hajiwezi.
Akizungumza na Amani, Kadinda alisema kuwa mwanamke anayemuoa si aliyezaa naye mtoto bali ni mwanamke aliyekuwa naye kwenye uhusiano kwa muda mrefu na tayari anatambua tabia zake hivyo hana shaka juu ya kuishi kwao pamoja.
“Wazazi wako tayari juu ya hilo nadhani na sitaki kumweka hadharani sasa hivi maana watu hawakawii kuharibu kwa maneno yao machafu, lakini wale ambao walidhani sitaweza kufanya hivyo watambue kuwa mwakani naoa,” alisema Kadinda.
~Source:Global Publishers

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini