Mgombea Uenyekiti na Mfanyakazi wake wauawa kwa kukatwa Mapanga


ALIYEKUWA mgombea nafasi ya Uenyekiti wa Serikali ya kitongoji cha Idodomiya kijiji cha Kanoga na mfanyakazi wake kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Kaliua mkoani Tabora, wameuawa kwa kupigwa kwa mapanga.
 
Katibu wa chama hicho Wilaya, Rajabu Hamisi alisema kuwa mauaji hayo yalitokea juzi nyumbani kwake katika kijiji cha Kanoga wilayani Kaliua mkoani hapa.
 
Alimtaja aliyekuwa mgombea wao aliyeuawa kuwa ni Wilsoni Masanilo (35) mfanyabiashara wa ng’ombe na mfanyakazi wake ni Juma Ujege (30).
 
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, Suzana Kaganda alikiri kuwapo kwa mauaji hayo na kusema taarifa za awali zinaonesha kwamba wameuawa na majambazi waliokuwa wanatafuta fedha walizokuwa wameuza ng’ombe.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini