Ukawa Mkilifanya Hili, 2015 Mnashinda kwa Zaidi ya 80% na Kuingia Magogoni Kiulaini

Awali ya yote niwatakie heri ya X-MAS.
Katika sehemu ambayo ilisahaulika na kudharaulika katika nchi hii ni ngazi ya local government. Tumekuwa tukiishi kwa muda mrefu uku tukimaanishwa kuwa Wenyeviti wa serekali za mitaa/vitongoji ni wazee tena wale ambao hawana cha kufanya na zaidi ni wale wazee wasiokuwa na elimu ya kutosha. 
Kwakua Ukawa safari hii imechukua viti vingi kwenye ngazi ya Serekali ya mitaa. Wito wangu kwa Ukawa ni kutoa semina elekezi kwa wenyeviti wote na wajumbe waliochaguliwa katika mitaa husika. 
Ki ukweli wenyeviti wengi wa serikali za mitaa toka Ukawa ni wasomi ila ni wageni katika mambo ya Local Government hivyo basi kuwaacha waanze kazi zao bila kuwapiga msasa itawafanya wafanye kazi kama wenyeviti wa ccm walivyokuwa wakifanya before. Ila wakipatiwa mafunzo watafanya kazi kiufasaha na hatimae yale mabadiliko yaliyotazamiwa na wananchi yataonekana.
By Eddo Sambai

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini