Mashabiki walumbana kuhusu video ya Alikiba ‘Mwana’, kama ni sawa au si sawa kwa video kutofuata maudhui ya wimbo

Wiki moja baada ya video ya Alikiba ‘Mwana’ iliyofanyiika Afrika Kusini na kuongozwa na Godfather, itoke, kumekuwa na maoni tofauti kuhusiana na video hiyo. Baadhi yao wameonekana kuifurahia na wengine wameonekana kutoridhishwa na baadhi ya vitu.

Baadhi ya waliotoa maoni wamesema kuwa walitegemea kuona video yenye script inayoendana na maudhui ya wimbo ili kumuwezesha hata mtu asiyejua kiswahili kuweza angalau kuelewa kwa kutazama vitendo, huku wengine wakitetea kuwa si lazima kila video iwe na tale inayoendana na wimbo.

Haya ni baadhi ya maoni ya walioitazama video hiyo kupitia channel ya Alikiba Youtube ambayo hadi sasa ina views 185,005:

king dady
video iko swafi sn, ila k2 kmoja cha kurekebsha, ujue bana music ni luga ya wote, yan kwmba wimbo ukiwa sawa na baadhi ya matukio ya kweny videoo kidg inasaidia ht km wacojua swahil wanaelewa ulichoimba kw kutizama video, hapo kw wacojua ulichoimba wataona swafi, ila kw tunaojua ulichoimba kiuukwe bnafsi ckutegemea km hii video ingekuja kuw hivi… NLICHOPENDA NI KWAKUA UMEENDA KUFANYA KWNY PRODUCTION KUBWA, ila hukukua na maelewano mazuri kat yawew na director wa hii video .. next time try 2 do somthing better, yt ya yte mzik wa africa lzm ukue

john senior
kiukweli video ni kali kwa alikiba na anajitahd kulitafta soko la kimataifa ila maudhui ya wimbo hauonekani kabisa kwenye video yaan kwa mtu asiyejua kiswahili ukimwambia hii nyimbo ina ujumbe mkali lazima apinge nimegundua ali alikamia sana kuifanya video hii ndo maana yametokeA all in all ni mtazamo wangu kama shabiki

mchikirwa ndelejai
Those who want the video to have a tale line the same as the song,this aint a movie bana…….Hayo yalipitwa na wakati,u sit n enoy the video, and stop comparing diamond to kiba or vice versa,they are their own artists n they all have reache where they are by merit!!

Eloi Laban
THE FACT IS WHOEVER DOESN’T UNDERSTAND SWAHILI… ENJOY THE DANCE. PERIOD! THIS VIDEO QUALITY I CAN SAY IS THE BEST EVER DONE

IBRAHIM PRIVATUS
HAPO NDIPO KILA SIKU ALIKIBA UNAKOSEA NA UNAONEKA BADO SANA KWANINI UNAKURUPUKA? UNAWAUMIZA MASHABIKI WAKO NA KUWAANGUSHA VIBAYA SANA YAANI HUU WIMBO SI WA DANCE HUU WIMBO ULITAKIWA UWE NA VITENDO NDANI YAKE YAANI MAUDHUI YAMEPOTEA KABISA NA UMEFANYA VIDEO IONEKANE

Geofrey Adroph
Uzuri wa wimbo ni tofauti sana na mwonekano wa video maana nilitegemea kuona binti ambaye anatumia madawa na istoshe tena analewa hapo ndo ningeona dhima ya huu wimbo inabidi ujipange sana Bro

athuman gullam
Watu wabadilike na kuweka chuki zao mbali, huu ni music sio movie ambayo inaonyesha kila tukio lililoandikwa…ebu angalien video za wanamuziki wakubwa dunian wanafanya nn sio kulaumu na kukosoa msivyo vijua …eti video haiendan na maudhui ya nyimbo nk. Angalieni video kama NEW FLAME, SHOULD HAVE KISS YOU,ROYAL hizo ni mfano tu wa videos za Chris brown na zinabamba kila kona ya dunia …Alikiba u did well with ur btful video n everything inside it is good .toeni video zenu tuone # HATERS #

alex mbuli
Honestly…hii video siwez angalia Mara mbili..inaboa.. kwa msanii mkubwa kama wew tunatarajia mambo makubwa pia toka Kwako…Ila kwa hapa umekurupuka sana kaka..kipaji cha kuimba unacho..Ila wew sio msanii..video yako haiendani na maudhui..Ingawa quality ni nzuri…kwa ushauri tu naomba mshirikishe diamond na ukubali yeye kakuzidi kiusanii..mtatoa Kitu Kizuri sana

IDP MUZIQ
I am a musician n ur number one fan from Kenya,honestly u tried but hata hivyo still theme ya song haimbatani na video if i were u ninge do away with this video n do it again before its too late.halafu pia fanyia video kama hii TZ coz south Africa hata hawelewi unachozungumzia kisha ungewashirikisha wale madancers wako wa serengeti fiesta otherwise competition ni noma

Julius Mbungo
BIG UP ALI KIBA.. video ni kali sana.. wanaosema haijaendana na maudhui ya wimbo hawajielewi na wanaongea kwa ushabiki.. acheni mambo ya diamond hapa.. yeye anafanya yake na kiba mwachen afanye yake.. nyie wapumbavu ndio mnaoleta fitna kwa kulinganisha watu.. the video is nice.. angalien nyimbo kibao mbele sio lazima ziendane na maudhui mfano mzuri ni loyal ya chris brown mnaona maudhui kwenye video pale au?? shut yo mouths kama hamna cha kuongea

hyme chicco
Video nzuri sana…Maana ya hii video ata wasio elewa kiswahili wa delight in the dance,kwasababu nyimbo ni ya kuchezeka!

Dotto Kahindi
Wimbo unamzungumzia binti aliyeloweza Dar halafu video inaonyesha mitaa ya Afrika Kusini, unajua hawa maproducer wa video wasiwafanye wasanii wa bongo kuwa watumwa, yaani nimeumia sana, nilitegemea kumwona huyo binti na mikasa iliyomkuta lakini kiukweli umeniangusha sana

deo alphonce
Nice video ,japo watu wnalalamika hakuna tale but creativity ya pale club. Iko poa sana

Imani Tutu
Mchizi video iko bomba sana ila Naona bado unazunguka palepale, nikiiyangalia Iyo video nikama na iyangalia ile ya ommy dimpoz (ndagushima) japokuwa ni thought tofauti. fanyagarama alafu kitu kionekane ila sio kwasababu umefanyia nje ya nchi tu!!

fred eugene
Tusiwe wazee wa kukariri Video NZURI,HApo Hamjaona Tale Ndo Maana mmeona mbaya Hamjui kwel yan….@VANESSA MDEE-HaMJUI Mbn Tale Haijaendana AU…
Tusiwe WANAFKI……Pia Shabikia MZIKI Sio Mimi @Team Kiba Mimi @Team Diamond UFALA Huo…Aya Bhasi Next Time Preside over wewe.
Penda au Usipende Nzuri.

nicolas jonathan
Ushauri tu kwa wanaotaka maudhui. “sikuizi mziki ni mpana sana na maigizo ya kibongo ni mmziki wa zamani,, skuizi tunatka kitu unique ambacho hawajfnya watu weng ndo kitutoe. Kwaiyo we kma ulikua unasubiri movii imekula kwko afu usitake mtu atoe video unayoitaka weee…. By the way its butful video

Piter Asifa
Video iko poa tatizo ppl wame kariri sio lazma iende kwa matukio sio movie hiyo hiyo ni Video ya nyimbo as friend apo # omonyi alivo ongea

ibrahim masoud
kiba ndio amekosea hii video, lakin uaweza ukaotea uelekeo wa iyo vdeo. kma angefkiria kuweka mtoto wa iringa alie kimbilia dar ingekua nibonge ya uupuz goal nikuiona mtv, trace na channel kubwa ulimwenguni. chukulia hii ni moja ya zile video ambazo huelew znaongelea nn ila tunazpenda, kma ngapi mnajua maana ya skelewu lakin cheki kideo hutaki kujua amnongelea nn

neysha keys
video iko kawaida mo than the expectations. ukwel usemwe kwan yy nan bna. vdeo nying ambazo haziendan n maudhui labda za kizungu co za kiswahil o africa probably zA RAP. quality iko poa mmevaa fresh lkn content 0. muandika scripts hajakua thoughts vzr. but ucjali utafka level zile jikakamue hlf kaa na walio top utafanikiwa 2

Henry Tudor
Mnataka maudhui yapi sasa izo ni video za kizaman mtu anavuta madawa ya kulevya anaoneshwa au mnataka iwe kma mac muga anaonekna ana kula bata sauz?mbna dimond kvaa kma shakazulu kwny vdeo ya mdgmdgo na wakat wmbo ni maadhi ya tz sio sauz kjaza na wazngu tu mle kitolondo cjui ndo yle mzngu ata atumwon,videeo kali bhana alikiba pop it in niqqa

Annarisa Peter
video nzuri sana,, baada ya watanzania kusifia vitu vizuri si ndo wa kwanza kwa majungu! let us support what is ours tuache chuki binafsi kwenye maendeleo! ukiulizwa kwa nini unamchukia m2 jibu huna! if you don’t like someone omba Mungu akusaidie umpende cyo kuendeleza chuki haijengi, hautafika mbali kamwe. Go kiba Mungu atakupigania.

Abdulaziz Raha
Let me tell you mtu anapofanya kitu na kinapokuwa hakipo sw na ukampa ushauri haimaanishi kwamba unamchukia… kusema kweli quality, mavazi vyote vipo poa tatzo maudhui hayaendani na nyimbo… ali kiba ni msanii wetu waTanzania ss anapokosea sisi tusipomrekebisha tutakuwa hatumjengi… Tanzania one

FARAJI MWANJA
sasa tunaangalia quality video angalia video nyingi za nje sikiliza kwa makini alafu angalia na video kama zinaendana mambo ya kizamani hayo ndugu

kazungu mabeyo
wimbo huu haujatendewaa hakii , video ya kawaidaa sanaa, sikutegemeaaa kama itakuwaa ya kawaidaa namnaa hiii, but it is the good start let hope for best videos in prospect… always on yourside king kiba.

Airborne Films
ALI KIBA HAS DONE IT GREAT. THIS VIDEO DESERVES AN AWARD. IT WAY MUCH ABOVE STANDARDS. ITS YOUR RESPONSIBILITY AS A VIEWER TO RELATE TO IT. BUT DONT EXPECT ALI KIBA TO DO SOMETHING ACCORDING TO WHAT TANZANIANS WANT. UNDERSTAND THAT MUZIK IS AN ART AND NOT LIMITED TO CREATIVITY AND QUALITY.
SO PEOPLE NEED TO THINK FIRST BEFORE ARGUING ON A VIDEO YET THEY ARE NOT EITHER FILM MAKERS OR VIDEO DIRECTORS.
GOOD STUFF ALI KIBA. I GIVE IT 10/10. U R GONE INTERNATIONAL AND THATS THA WAY IT SHOULD BE.

Alex Kasangaya
Video ni mzuri and ofcoz inachezeka kiclub and anywhere… ila ukisema chrbrwn katoa loyal vdeo wth no content thn unataka alikiba afanye hvyohvyo while yeye kiba anatafuta int market utakuwa wakasoea…… CB z arleady knwn worldwide…… ushauri wangu on vdeo re do it bong0 with content in it and fantastic dancers esp ladies

Clarence John
IT IS ONE OF THE BEST VIDEO from KIBA ever been before!… tunakosea sana tunapomlaumu Kiba kwa suala la SCRIPT..mi nadhani ni makosa ya DIRECTOR!….angeimba OFF KEY hapo tungemlaumu kiba kwa kutojua kuimba!…lakini suala la VIDEO anaetakiwa kulaumiwa kwanza ni DIRECTOR..alafu sio kila kitu kiwe kwenye SCRIPT sio BONGO MOVIE hiyo…Aliyemshauri akafanye video kwa GODFATHER ndio alimuingiza choo cha kike..huwezi kwenda kwa rafiki wa ADUI wako ukategemea atakushauri vizuri ili umuangamize adui yako ambae kwake ni swaiba!..

claudy muhala
Wengine wameelewa wengine hawajaelewa, ila yote ni taswira halisi ya jinsi ulivyofanya vizuri na jinsi ulivyoboronga. Sisi humu wengi ni mashabiki wako na kikubwa sio tu ni mashabiki lakini tunakupenda na kutaka kuona unatoa kitu kizuri. Unajua hii nyimbo imetoka kitambo na watu wanaifanhamu na waliisubiri kitambo sana ila walitegemea kuona dhima halisi ya nyimbo

Rasheed Rai
The song is fantastic…I just feel that Kiba would have done better than this on the video.
I like the audio more than the video. GodFather lacked some creativity on the concept of this video. I don’t see the subject of the song in this video.

MAGESA JOSEPH
Kichupa kipo poa sana af umekuja na style yako mpya safi kiba ila maudhui na chupa vpo opposite bro huu mziki co wako ni wataifa zima xo ww unatuwakilisha na tunataka uwakilishe vyema zaidi

Cecy Steve
Ni mbayaaa haiendani kabisa na maudhui mara mia angefanya kama tale kidogo ndani kucheza kwenyewe hajui

Lelo kaka
WABONGO HATUELEWI MAANA YA MAUDHUI. AND THEN HATUNA MAAMUZ YASIYO SAHIHI HIVI MTU KAKAKURUPUKA TU AND THEN ATOE KITU KIBOVU EMB KUWEN WAELEWA VIDEO INA UJUMBE ILA SISHANGAI SHULE NI NDOGO NIKAMA WATOTO KILA KITU MTAFUNIWE. MSIKURUPUKE FATILIEN KWAMAKIN MJUE ANACHOKIMAANISHA

Azeez S.A
Script mbovu…hii video itaupoteza wimbo. Wimbo ni mkali sana kuliko video. Halafu huyu God Father ambaye watanzania wengi wanamkimbilia huko South mbona wa kawaida tu. Tunajua ana connection na vituo vikubwa vya TV Afrika na pia ana quality nzuri picha. Kama hizo ndo sababu za kumkimbilia basi wasanii wanapaswa kuandaa script wenyewe. Wasanii mnapaswa kutake control ya video zenu, maana zikiharibika hasara kwenu.

Tariki magowa
Halafu siyo kila k2 muige kwenda kwa GODFATHER vingene fanyeni hapahapa home na itapendwa2. sio mnakwenda kuwasumbua wa2. wanaacha kazi zao za maana mnapeleka ujinga. ole wenu mludie tena na sio ww2 brather kiba bali ni wale wote wanao taka kwenda kupeleka ujinga kwa GODFATHER. sory ni mtazamo2

Mwinjuma Lukwar
kiukweli nisiwe mnafiki huyo mwana sijamuona anaye semwa hapo maana sioni uhusiano wa wewe kujiangalia kwenye kioo na kumtaja mwana aliye pagawa na anasa za mjini ,,hey kaka badilika ndugu uadui tuweke pembeni kubali kujifunza maana inaelekea hutaki kujifunza na ndo maana hata instagram hujafollow mtu hata mmmoja hiyo imejidhihirishaa ona sasa unatuangusha mashabiki wako good quality but contentlessss

ASHER OMONDI
This guy Godfather production Im yet to be with you why East African musicians rush to him for the video productions! Look, the video runs for 2 minutes before you see any lady map who should have been the main character here.The theme in the song is way sooooo different from what is in the flick!! It is all about Ali Kiba and the theme “LOVE” in it is lost.BORINGLY BORING!!!1

Wewe una maoni gani? Andika chochote hapo chini.
~Bongo5

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini