BUBU Afanyiwa Unyama wa Kutisha......Wanaume Watano Wamteka na Kumbaka kwa Zamu

MKAZI wa kitongoji cha Chingale, kijiji cha Mtakuja kata ya Temeke katika Halmashauri ya mji wa Masasi mkoani Mtwara ambaye ni bubu, Asumini Fakihi amebakwa na watu watano wasiojulikana na kumsababishia majeraha na kulazwa katika Hospitali ya Mkomaindo mjini Masasi.
 
Kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara, Agustino Ollomi alisema juzi saa 1:00 usiku wa mkesha wa Krismasi katika kitongoji cha Chingale, mama huyo alivamiwa na watu hao wasiofahamika waliofanikiwa kumfanyia kitendo hicho na kutokomea kusikojulikana.
 
Mwanamke huyo hakuweza kuwatambua watu hao mara moja na kwamba baada ya tukio hilo Mwenyekiti wa kitongoji hicho, kwa ushirikiano na wasamaria walitoa taarifa kituo cha polisi Masasi kwa msaada zaidi.
 
Ollomi alisema polisi walifanikiwa kufika katika eneo la tukio usiku huo wa mkesha wa Krismasi na kukuta mama huyo (39) akiwa hajitambui huku sehemu zake za siri zikiwa na majeraha makubwa na kukimbizwa katika hospitali ya Mkomaindo ambako hadi sasa amelazwa akipatiwa matibabu.
 
Alisema jeshi la polisi mkoani Mtwara linaendelea kuwasaka watuhumiwa hao na watakapopatikana watafikishwa mahakamani kujibu shitaka hilo linalowakabili.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini