MWALIMU KUDAIWA KUNYONGA MTOTO GESTI, MWILI WAHIFADHIWA KWENYE KORIDO HOSPITALI HAINA MOCHWARI

Jeshi la polisi wilayani Mbogwe mkoani Geita linashikilia mwalimu wa shule ya msingi Kasandalala wilayani humo Laideth Constantine mwenye umri wa miaka 33 baada ya kumnyonga mwanae wa kiume mwenye umri wa miaka 7 akiwa kwenye nyumba ya kulala wageni(Gesti).

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana ambapo 
 kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa geita Joseph Konyo amesema tayari wanamshikilia mtuhumiwa baada ya vipimo vya daktari kudhibitisha kuwa mtoto huyo kanyongwa.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema mwalimu huyo amekuwa na mambo ya kushangaza jamii kwani wakati mwingine anajifanya mlokole,mara anakuwa mkali na kugombana na kila mtu hasa wakati akiwa shuleni.

“Tumekuwa tukimshangaa mwalimu huyu,kuna wakati anakuwa mlokole,wakati mwingine anakuwa,mtaratibu sana,sisi tunashangaa sana kutokea kwa tukio hili”,walisema.

Kwa upande wake mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Mbogwe mkoani Geita Cosmas Kilosa amesema vipimo vinaonesha  kuwa mtoto huyo amefariki dunia kwa kunyongwa.
Na Philip Chimi

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini