MAMA MJAMZITO ASHIKWA NA UCHUNGU KWENYE TRENI, POLISI WALAZIMIKA KUMZALISHA

Katika siku ya christmas watoto wengi walizaliwa katika siku hiyo, lakini mtoto huyu alizaliwa mazingira ambayo wengi walionekana kushangazwa. 

Maafisa wawili wa Polisi Daniel Caban na Darrell James walipewa taarifa ya kutakiwa kutoa msaada wa dharura katika treni ya abiria Philadelphia, walipofika waligundua kwamba dharura yenyewe ni mwanamke ambaye alikuwa katika hali ya kukariba kujifungua, muda haukuruhusu kumkimbiza Hospitali.
Walimsaidia mwanamke huyo kujifungua salama mtoto wa kiume na baadaye wakapelekwa Hospitali ya Hahnemann University wote wakiwa na hali nzuri.
Afisa mmoja amesema alikuwa ameshafungua zawadi zake zote kwa ajili ya siku hiyo na hakujua kama kuna zawadi nyingine ambayo ilikuwa inamsubiria aifungue.
Tukio kama hili liliwahi kutokea mwaka jana baada ya mwanamke mmoja kujifungua mtoto wa kike akiwa kwenye treni ya abiria London lakini yeye alipata bahati ya kusaidiwa na mkunga ambaye alikuwa ndani ya treni hiyo pia.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini