Gari linaloweza kujiegesha kwa kutumia saa
Hakuna kitu kibaya kama kusahau ulikoegesha gari lako katika jengo la kuegeshea magari lenye goraf nyingi.
Lakini
hivi karibuni hautahihajika kupanda gorofa kutafuta gari lako kwani
kampuni ya kutengeza magari ya BMW, imetangaza kuzindia kifuaa ambacho
kinaweza kuyawezesha magari ya kampuni hio kujiegesha yenyewe kwa
kubonyeza tu kifaa hicho.Hata hivyo dereva wa gari hilo atalazimika kuvaa saa ya Smartphone mkononi ambayo ataibonyeza na kuiamrisha kwa sauti gari hilo kwenda kujiegesha.
Tawi la kampuni ya BMW mjini Munich, Ujerumani limezindua teknolojia hio ambayo inawezesha gari kujiegesha lenyewe.
Gari hilo linatumia miale ya Leser iliyo kujitafutia ramani ya jengo ambalo lipo. Dereva anaweza kuliamrisha gari hilo kwenda kujiegesha kwa kutumia Smartphone.
Badala ya kutumia GPS, teknolojia hio inatumia miale ya Laser ambayo hutengeza ramani inayolisaidia gari hilo kutafuta sehemu ya kwenda kujiegesha.
Teknolojia hiyo inaiwezesha gari hilo kuona njia na nafasi ya kujiegeshea na pia kuona vizingiti mfano kama magari ambayo hayajaegeshwa vyema.
Kwa mujibi wa waliotengeza gari hilo, linaweza kujitafutia nafasi ya kujiegesha na hata kuweza kutambua sehemu ambako kuna nafasi.
Teknolojia hio inatengezwa sambamba na teknolojia nyinginezo zitakazoweza kuzuia gari hilo kugongana na magari mangeine.