BIBI KIZEE ADONDOKA NA UNGO AKITOKA KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA KRISMAS HUKO KAHAMA
Wakazi wa
Bukondamoyo katika Halmashauri ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga wameingiwa na
hofu baada ya bibi kizee mmoja kudaiwa kudondoka kwenye ungo akidaiwa kutoka
mkoani Tabora kusherekea sikukuu ya Chrismas.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo
lililokusanya umati mkubwa wa watu wamedai bibi kizee huyo alidondoka alfajiri
huku akidai alikuwa na wenzie watano ambao walifanikiwa kutoroka kuelekea
kijiji cha Ndugu kata ya Kinaga wilayani Kahama.
Aidha bibi kizee huyo baada ya kuhojiwa na mwandishi
wa habari hizi alisema anaitwa Chausiku huku akidai alikuwa akielekea katika
kijiji hicho cha Ndugu.
Hata hivyo jeshi la polisi wilayani Kahama
liliwahi kufika kwenye tukio na kumuokoa bibi kizee huyo ambaye alionekana
kuvaa nguo zilizochakaa na makovu katika mkono wake wa kushoto ambapo imedaiwa
alichubuka wakati akidondoka.
Tukio hilo limehusishwa na imani za
kishirikina kwa kuwa ungo ni kifaa kinachoaminiwa kutumika kwa nguvu ya giza
kupaa angani kama usafiri unaotumiwa na wanga katika shughuli zao za nguvu ya
giza ikiwemo uchawi.