MAMA AMUUA MWANAYE WA KUMZAA ILI AENDE MBINGUNI linsey

linsey
Mwanamke mmoja nchini Marekani ameamua kumuua mwanaye wa kiume wa miaka 10 akiamini ataenda mbinguni na kukwepa matatizo ya dunia.
Mwanamke huyo mkazi wa mji wa Kansas Lindsey Blansett mwenye miaka 33 alifunguliwa mashtaka ya mauaji baada ya kutenda kosa hilo kwa mtoto huyo aliyejulikana kwa jina la Caleb wakati wakiwa nyumbani na dada yake.
caleb
Lindsey Blansett na mwanaye Caleb enzi za uhai wake
Polisi walisema mama huyo alimkata mtoto wake kwa kutumia kisu bila kujali maumivu aliyoyapata na baada ya kutenda kosa hilo aliwapigia polisi simu ili waweze kumshtaki.
Alisema alikua tayari kutumikia adhabu yoyote ile ilimradi ametimiza lengo lake la kumuua mwanaye na kuamini ataenda Mbinguni na kukwepa matatizo ya kidunia ambayo angekutana nayo siku za baadaye.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini