MAJANGA MWISHONI MWA MWAKA 2014: NDEGE YA AIRASIA QZ8501 YAPOTEA IKIWA NA WATU 162

Ndege ya AirAsia, QZ8501iliyopoteza mawasiliano ikiwa na watu 162 ikitokea Indonesia kwenda Singapore.
Ndugu, jamaa na marafiki wa abiria waliokuwa kwenye ndege ya AirAsia QZ8501 wakiwa na majonzi wakati wakisubiri taarifa kuhusu ndugu zao katika Uwanja wa Ndege wa Surabaya, Indonesia.
NDEGE ya AirAsia, QZ8501 iliyokuwa na watu 162 ikitokea Indonesia kwenda Singapore imepoteza mawasiliano leo asubuhi.
Kati ya watu hao 162, abiria walikuwa 155, marubani 2 na wafanyakazi wa ndege hiyo 5. Watu 157 ni raia wa Indonesia, 3 raia wa Korea Kusini, 1 kutoka Malaysia na 1 raia wa Singapore.
Imeelezwa kuwa kabla ya ndege hiyo kupoteza mawasiliano, rubani aliomba kubadili uelekeo wa kawaida kutokana na hali mbaya ya hewa.
Ndege hiyo ilifanyiwa matengenezo kwa mara ya mwisho Novemba 16, 2014 kama ilivyokuwa imepangwa.
Rubani wa ndege hiyo ana uzoefu wa saa 6,100 angani huku msaidizi wake akiwa na uzoefu wa saa 2,275.

Miongoni mwa abiria 155 waliokuwa kwenye ndege hiyo, 138 ni watu wazima, 16 watoto na 1 mama mjamzito.
QZ8501 imetoka Indonesia saa 11: 27 alfajiri na ilitarajiwa kuwasili Singapore saa 2:37 asubuhi.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …