Rose Ndauka Awapasha Wanaofuatilia Maisha Yake...Kisa Namkasa? Picha Hizi!!

Rose Ndauka ambae ni mama wa mtoto mmoja amewatolea uvivu baadhi ya watu ambao ni “followers” wake kwenye mtandao wa Instagram ambao walimshambulia sana kwa maneno baada ya yeye kuweka picha hiyo hapo juu akiwa amekaa na “jamaa” huku amemfunika uso.
Chokochoko
Baadhi ya watu hao walichukulia kwamba huyu jamaa pichani ndio “PROJECT” mpya ya Rose hivyo wakaanza kumshabulia mwananadada Rose kwa maneno kuwa hajatulia na ndiomana aliachika kwa bwana, na wengine wakisema kwa yeye kwasasa anamtoto mdogo kwa hiyo inampasa atulie na amlee mtoto kwanza na sio kufanya maswala kama hayo... na mengine mengi tu. Huku “followes” wake wengi wakionekana kumuunga mkono Rose kwa alichoonekana kukifanya kwani ana haki ya kufanya kile roho yake inapenda, hivyo basi ni vyema watu wamuache na waache  “PROJECT” iendelee.
Rose Awashukia
Baada ya figisufigisu yote hiyo hatimaye Rose mwenye alifunguka kama ifuatavyo;
“instfamily love them so much#ushauri mdogo kwa wale wanaopenda kuwapangia watu namna ya kuishi,tafutene ofisi ili tuweze kuja na kuwaeleza ili mkiwa mnatupangia uwe unajua vizuri kuhusu mtu husika sio kukurupuka tu,acheni ushamba duh mnanichosha kwakweli.Tag mtu yeyote mwenye tabia ya kukurupuka na kuongea asichokijua loooh”
Nadhani ujumbe umefika.Sina neno lakuongeza hapo


 

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini