UMEISIKIA HII YA WALE WATUHUMIWA WALIOMUUA DKT SENGONDO MVUNGI?

Hilo lilitokea jana saa nne asubuhi ,muda mfupi baada ya wakili wa
serikali,Peter Njikekumweleza Hakimu Hellen Liwa kuwa kesi hiyo ilifika
mbele yake kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi wake bado
haujakamilika na kuomba ipangwe tarehe nyingine.
Mshtakiwa Masunga Makenza alidai hafahamu sheria ,kesi hiyo ni ya
muda mrefu na akahoji jalada likienda kwa DPP linatakiwa kukaa kwa muda
gani.
Makenza alidai kuwa kesi hiyo ni ya kubambikiwa na kwamba ingekuwa
halisi,upande wa mashtaka ungekuwa umekwishakamilisha upelelezi na
kwamba wapotayari kushtakiwa ila kama upande wa mashtaka umeshindwa
kukamilisha upelelezi mahakama iwaachie huru na ikikamilisha iwakamate
tena.