MKOANI NJOMBE! MUUMINI AFUNGULIWA KESI YA UTAPELI!

KURUGENZI wa Bendi ya Double M
Sound, Mwinjuma Muumini ‘Kocha wa
Dunia’, amefunguliwa kesi kwa jalada
namba; NJ/RB/4150/2014 madai
KUTOKUWEPO ENEO LA TUKIO na
kukiuka masharti ya mkataba ya kufanya
shoo mkoani Njombe.
Mwandaaji wa shoo hiyo iliyofanyikia
Ukumbi wa Day to Day, Sylvia
Mwakkikufi akizungumza na Amani juzi,
alisema amefanya hivyo baada ya
Muumini na bendi yake kutokea
ukumbini saa nane usiku Jumamosi
iliyopita akiwa na kufanya shoo kwa
dakika 35 tofauti na muda wa mkataba.
“Licha ya kuchukua pesa yangu na
kutofanya kazi, kapoteza muda wangu,
kanishushia hadhi, kanikosanisha na
wadhamini,” alisema. Sylvia ambaye ni
mwandaaji wa shoo mbalimbali mkoani
Njombe hivi karibuni aliandaa shoo na
kuiita Usiku wa Watoto Yatima.
Hata hivyo, asubuhi yake, Sylvia alisema,
Muumini alikamatwa na Polisi wa
Njombe na kuwekwa lupango kwa siku
mbili kabla ya kudhaminiwa. Kesi yake
itatinga mahakamani wakati wowote.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini