FLORA MBASHA: DVD MPYA YA NIPE NGUVU YA KUSHIDA SASA IKO MADUKANI

Mungu amekuwa mwema kwangu tangia nilipomkubari kuwa mwokozi wangu na nguzo yangu. Nimeona Mungu akinishindia na magumu ninayopitia na niliyoyapitia katika maisha yangu.




 Nimeona Mungu huyu unayemwabudu kila siku akinivusha na kunitia moyo pale ninapoona akili yangukufikiri jinsi ya kutatua yale yaliyombele yangu. Mungu huyu ni waajabu kwangu, kaniwezesha katika uaandaji wa albamu hii mpya ya "NIPE NGUVU YA KUSHINDA". Nazidi kumshangaa Mungu huruma zake na fadhili zake kwangu.Ninaamini hata wewe unaweza kufarijika na kuinua imani yako kwa kusikiliza ujumbe ulio ndani ya DVD hii. Mungu wangu anataka kuongea na wewe kwa kupitia uimbaji wangu. Ni maneno ya Mungu ambayo ameweka ndani yangu kwaajili ya kuponya na kuinua imani yako kwa njia ya uimbaji. Kwangu ni vigumu mno kukufikia na kukuhubiria habari njema, lakini kwa kupitia DVD hii utaweza kuungana nami na kupata Neno la Mungu.




Ndugu mpendwa wangu, ninatambua unatamani sana kushinda magumu yaliyoko mbele yako na haya unayopambana nayo, na umekuwa ukijiuliza nitafanya nini? Lakini natamani kukutia moyo na kukuomba uzidi kuwa magoti mwa Mungu wetu kila kuitwapo leo. Acha kusikiliza maneno ya watu wanaokusemea mabaya ila msikilize Mungu wako naye atakutia nguvu. 


Nyimbo zilizomo humu zitakusaidia sana katika maisha yako haya. Mungu akubariki sana.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini