NEWS ALERT: MIILI YA WATU 14 WALIOFARIKI KATIKA AJALI YA MELI YA CONGO YAIBUKA KIGOMA, ZAZIKWA NA SREKALI YA TANZANIA
Na Editha Karlo Globu ya Jamii,Kigoma
JUMLA ya maiti 14 zimezikwa baada ya makubaliano baina ya serekali ya Tanzania na serekali ya Demokrasia ya Congo(DRC)ambapo katika mazishi hayo serekali ya Congo iliwakilishwa na Balozi wa Congo kutoka ubalozi mdogo wa DRC Mkoani Kigoma.
Akizungumza muda mfupi baada ya mazishi ya raia hao Balozi mdogo wa DRC nchini kutoka Ubaozi mdogo Mkoani hapa,Mh. Riki Moleme alisema.
Mh. Maleme alisema kuwa amefarijika sana kwa namna serekali ya Tanzania ilivyochukulia kwa umuhimu mkubwa swala la maafa hayo ya Raia wa Congo na namna ilivyojitoa kushughulikia mazishi ya miili hiyo
Naye Mhifadhi wa mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mahale,Herman Batiho alisema alianza kuona miili ya watu majira ya jioni ya Desemba 20 Mwaka huu na ndipo walipoamua kutoa taarifa katika mamlaka mbalimbali ambapo waliwasiliana na uongozi wa kijiji cha kalilani ambapo uongozi wa kijiji kwa kushirikiana na wanachi walianza kazi ya uopoji wa miili.
Mwenyekiti wa kijiji cha Kalilani,Songoro Saidi alisema kuwa waliona moja ya mili wa maiti hizo asubuhi ya Desemba 21 ukiwa umeibuka juu,pia walipata kuwepo kwa miili mingine ikiibuka na kuelea ndani ya Hifadhi ya Mahale na ndipo waliposhirikiana kuipoa miili hiyo na hadi kufanikisha mchakato wa mazishi.
Desemba 12 mwaka huu ya watu 128 walifariki dunia na wengine 250 waliokolewa kufuatia meli waliyokuwa wakisafiria kutoka Mobaa kuelekea Kalemii kuzama katika mwambao mwa ziwa Tanganyika katika Mkoa wa Kalemii nchini DRC

,Askari wa jeshi la ulinzi wa Tanzania(JWTZ)wakiwaongoza viongozi wa
serekali ya Tanzania na Congo na viongozi wa kijiji cha Kalikani pamoja
na wananchi katika mazishi ya raia 14 wa Jamuhuri ya kidemokrasia ya
Congo(DRC) waliofariki katika ajali ya meli Desemba 12 mwaka huu katika
Mkoa wa Kalemi na miili yao kuibuka katika Hifadhi ya Mhale.Picha na
Editha Karlo wa Globu ya Jamii, Kigoma
Michuzi