FISI AFUNGA MITAA MJINI SINGIDA, WANANCHI WATIMUA MBIO NA KUTELEKEZA NYUMBA ZAO

Katika hali isiyo ya kawaida wakazi wa manispaa ya Singida
wameingiwa na taharuki na kuanza kukimbia ovyo baada fisi
kuonekakana katikati ya mji wa Singida akiwa anakimbia na
kuingia katika maduka ya wafanya biashara.
Wakieeleza kwa hisia tofauti baadhi ya wakazi huku wengine
wakiwa wamepanda juu ya mapaa ya nyumba pamoja na watoto
wao kwa hofu ya kuumwa,wamesema kuonekana kwa fisi mjini
katikati ni jambo la ajabu kwani wanyama kama hao honekana vijiji
au porini,wengine wamesema labda mnyama huyo amechelewa
kurudi vichakani wakati alipokuwa amekuja kula mabaki ya chakula
mjini.
Akielezea tukio hilo Afisa maliasili mkoa wa Singida Bwana Charles
Kidua amesema pamoja na kwamba wanyama kama fisi wapo
katika manispaa ya Singida na pindi wanapo onekana katika
maeneo ambayo siyo ya kawaida ,Basi wananchi watoe taarifa kwa
mamlaka husika kwani wanyama kama haho wana weza kuwa na
ugonjwa wa kichaa ,badala ya kujichukulia hatua mkononi ya
kuwaua.
Kutokana na umati wa wananchi kuwa wengi wakati wakimfukuza
fisi huyo bila kujali askari waliokuwa wakituliza fujo huku wakiwa
na silaha,wanachi walifanikiwa kuwapokonya askari fisi baada ya
kumtega na kamba huku wakiimba tunataka fisi wetu na kuamua
kumkimbiza mjini huku wakimpiga umbali wa kilomita mbili.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini