UDSM yakanusha kumtunuku Diamond


Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimekanusha uvumi kuhusu kumtunuku msanii Diamond Platnumz shahada ya uzamivu (PhD) katika mahafali yake ya 44 yatakayofanyika Mlimani City, Novemba 8 jijini Dar es Salaam.
Chuo Kikuu cha  Dar es Salaam (UDSM) kimekanusha ujumbe uliopo katika mitandao ya kijamii ambao unadai kuwa msanii  wa kizazi kipya Naseeb Abdul maarufu kama Diamond atanukiwa Shahada ya Uzamivu  ya heshima katika mahafali ya 44 yanayotarajiwa  kufanyika Novemba 8.
Ujumbe huo ambao ulieleza kuwa Diamond atakabidhiwa  shahada hiyo sawa na aliyekuwa mkuu wa chuo hicho marehemu Balozi Fulgence Kazaura  katikati mahafali yatakayofanyika katikati ukumbi wa Mlimani City.
Akizungumzia habari hiyo, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Yunus Mgaya alisema hakuna kitu kitu kama hicho – ni uzushi.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini