ODAMA: NIKO KWENYE UHUSIANO MAKINI

MWANADADA mwenye mvuto wa kipekee ndani ya tasnia ya filamu Bongo, Jennifer Kyaka ‘Odama’ amefunguka kwamba kwa sasa yupo kwenye uhusiano makini (serious) na muda si mrefu ataolewa.

Mwanadada mwenye mvuto wa kipekee ndani ya tasnia ya filamu Bongo, Jennifer Kyaka ‘Odama’.
Akichonga na gazeti hili hivi karibuni Odama alisema: “Ukweli kwa sasa niko kwenye uhusiano siriasi na tuko kwenye mipango ya ndoa japokuwa siwezi kutaja mwezi au tarehe ila mashabiki watambue kwamba nitaolewa soon.”


Alipotakiwa kutaja angalau jina la mwanaume wake huyo, msanii huyo aliweka ngumu na kudai haina umuhimu kwa sasa hali inayoashiria huenda ni mume wa mtu na kwamba akimuanika atakinukisha.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini