Wema aonyesha jeuri ya pesa nchini China

WAKATI bebi wake, Nasibu Abdul ‘ Diamond Platnumz’ akiugulia maumivu ya kuzomewa
na mamia ya mashabiki wa muziki katika Tamasha la Fiesta jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wikiendi iliyopita , Wema Sepetu ‘ Madam’ anaponda raha ya maisha nchini China.

Chanzo makini kilicho ‘ kloz ’ na muigizaji huyo nyota wa filamu nchini , kimesema Wema alipaa na ndege ya Emirates wiki iliyopita, siku chache kabla ya Tamasha la
Fiesta, akiwa ameandamana na wanaume wawili, ambao ni meneja wake , Martin Kadinda na Petit Man , wote wakiwa wamekaa daraja la kwanza la dege hilo.

Chanzo hicho kilizidi kunyetisha kuwa gharama zote za safari hiyo zilibebwa na Madam mwenyewe na kwamba baada ya kufika katika jiji la Guangzhou nchini humo ,Wema na wanaume hao wawili walichukua
vyumba katika Hoteli ya Holiday Inn ,
inayotajwa kuwa moja ya hoteli ghali zaidi huko China.
“Yaani Wema jamani ana mambo,
inavyoonekana lile rhumba la wakati ule ameshalisahau, amesahau kabisa kama alishafulia, sasa Mungu kamjaalia kapata pesa anavyoitapanya ovyo mpaka roho
inauma . 

Wewe fikiria mtu amekwenda


kuchukua vifaa vya biashara , unakwenda na
hao wanaume wa kazi gani kama siyo kupoteza fedha tu , ” kilisema chanzo hicho.

Inadaiwa kwamba kilichompeleka Wema katika nchi hiyo yenye watu wengi zaidi kuliko yoyote duniani , ni ununuzi wa vipodozi , kwani ana mpango wa kufungua duka kubwa
katika eneo ambalo halijatajwa jijini Dar es Salaam.

Baada ya kufika huko, chanzo kinasema kuwa watu hao watatu wamekuwa wakiishi maisha ya starehe , wakila bata katika klabu
mbalimbali za usiku , ambako
wanajichanganya na watanzania wengine kuponda raha.

“Kwa matanuzi anayofanya kule , hata hiyo biashara aliyoifuata haina maana , angekuwa mtu mwenye nia ya biashara kweli , angetafuta tu hoteli ya kawaida ili kubana
matumizi aweze kuja na mzigo mkubwa, sasa wewe mwenyewe fikiria, hii wiki ya pili sasa ,
tena na wanaume wawili wanakutegemea , hizo pesa si kuzitapanya tu jamani , ” kilisema chanzo hicho kikionyesha kutofurahishwa na maisha ya staa huyo.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini