UNYAMA....BABU WA MIAKA 62 AMBAKA MJUKUU WAKE WA MIAKA MITANO HUKO MPANDA

Mzee wa miaka 62, Rashid Mbogo amepandishwa kizimbani katika
Mahakama ya Wilaya ya Mpanda kwa tuhuma za kumbaka mjukuu
wake mwenye umri wa miaka mitano.
Mtuhumiwa huyo, mkazi wa Kijiji cha Vikonge kilicho katika Kata ya
Mpandandogo wilayani Mpanda, alifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi
Mfawidhi, Chiganga Ntengwa na kusomewa mashtaka na
mwendesha mashtaka ambaye ni mkaguzi msaidizi wa polisi,
Naathaniel Silomba.
Ilidaiwa na mwendesha mashtaka huyo kuwa mtuhumiwa alitenda
kosa hilo Oktoba 19, mwaka huu saa 2:00 usiku akiwa nyumbani
kwake.
Mwendesha mashtaka huyo alidai kuwa siku ya tukio, mtuhumiwa
akiwa anasubiria chakula cha usiku wakati kikiandaliwa na mkewe,
alimwita mjukuu huyo na kisha kumpakata mapajani. Alidai kuwa
baadaye alivua nguo na kuanza kumbaka huku mtoto huyo akipiga
kelele za kuomba msaada kwa kitendo cha babu yake.
Mwendesha mashtaka huyo alidai kuwa baada ya kusikia mayowe
hayo, bibi wa mtoto huyo na majirani waliingia ndani ya nyumba na
kumkuta mtoto sebuleni akiwa anatokwa na damu nyingi sehemu
zake za siri huku analia kutokana na maumivu makali aliyokuwa
ameyapata.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo, mshtakiwa alikana mashtaka
hayo ambayo alikuwa amesomewa na mwendesha mashtaka.
Hakimu Chiganga aliieleza mahakama kuwa dhamana ya mshtakiwa
iko wazi endapo mshtakiwa atatimiza masharti.
Mshtakiwa alitakiwa awe na mdhamini mmoja mwenye mali
isiyohamishika yenye thamani ya Sh5 milioni.
Hata hivyo, mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti ya dhamana,
hivyo alipelekwa rumande.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini