UNAIKUMBUKA ILE YA CHID BENZ KUMTANDIKA RAY C? BAADA YA KUKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA RAY C AMEANDIKA HIVII.....

“Pole kaka yangu Chidi Benz,Naumia kuona tatizo uliokuwa nalo
bado haujalitaftia jibu unalijua la kutatua tatizo lako,Mimi ni dada
yako na tumeshafanya kazi Pamoja,Tatizo ulilonalo na Mimi
nilishakuwa nalo na niliweza kulitatua sababu nilijitambua na
kutafuta suluhu, nimejaribu kila njia kukushauri badala yake ukaja
na rungu la kimasai na kunitandika nalo nyumbani kwangu!
nadhani janga hili lililokukuta litakuwa Kama jibu kwako kwamba
unakoenda si salama kabisa kaka yangu ni bora ubadilishe njia ili
uweze kuungana nasi kwenye tiba ya Methadone kwani ndio Kiboko
ya madawa ya kulevya!!!!
Kama Mimi mwanamke nimeweza najua Hata wewe utaweza!!!!
Tanzania bila madawa ya kulevya Inawezekana !!
Watanzania tusimyanyapae Msanii wetu kwani Uteja ni ugonjwa
Kama ugonjwa mwingine na Unazuilika na Kutibika,Ana kipaji na
Ana uwezo wa kurudi tena kwenye Sanaa,Tumuombee mema………
Tanzania Stand Up n Wish Him Luck…………With Like,Ray C
Foundation.”

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini