PUNDA WAMFIKISHIA UJUMBE RAIS WA KENYA

 Wanaharakati wa Kenya wamewahi kutumia Nguruwe waliopakwa damu kuopnyesha ambavyo wanasiasa wa Kenya ni wafisadi
Hii leo kulikuwa na taharuki katikati mwa mji wa Nairobi baada ya Punda waliokuwa wamepakwa rangi kupatikana wakizurura mjini humo.
Walikuwa na maandiko katika mwili wao yakisema: 'Tumechoka'
Neno 'Tumechoka' ni kauli mbiu ambayo ilitumiwa na mashirika ya kijamii kuelezea wasiwasi kuhusu hali ya utovu wa usalama nchini kote.
 Baadhi ya wananchi walishangaa Punda walikuwa wanafanya nini mjini kumbe wanaharakati ndio waliowaleta huko kuonyesha uchovu wao
 Kauli mbiu hio ilitumiwa mashambulizi yalipofanywa dhidi ya wakenya mjini Mandera Kaskazini mwa Kenya ambapo wanaharakati walipiga kambi katika ofisi ya Rais wiki kadhaa zilizopita kulalamikia ukosefu wa usalama.
Kwa kutumia Punda, kupitisha ujumbe wao, ni dhahiri kuwa ujumbe wao umefika kwa wengi.
Wanaharakati hao, wamewahi kutumia Nguruwe kuonyesha walivyo walafi na wafisadi wanasiasa wa Kenya.
Punda hao walikuwa 22 na walifikishwa kati kati ya mji kwa Lori. Dereva wa lori hilo alisema kuwa alilipwa na mtu flani kupeleka wanyama hao mjini.
Lori hilo lilipofikishwa mjini, mwanamume aliyekuwa amekodisha lori hilo aliamua kutoka kwenye Lori na wanyama hao.
Polisi wamesema wanachunguza kujua nani waliofanya kazi hio.
Wanyama hao walinuiwa kutuma ujumbe kwamba wakenya wamechoshwa na hali mbaya ya usalama, alisema mwanaharakti mmoja aliyekuwa kwenye Lori hilo.
''Tumechoshwa na uongozi mbaya, '' alisikika akisema mwanaharakati mmoja huku akiwaskuma Punda hao kutoka kwa Lori.

Polisi wanasema wanawasaka wale waliohusika na kitendo hicho.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …