GK asema Diva ndiye mpenzi wake bora kuliko wote aliowahi kuwa nao


Rapper wa East Coast Team, King Crazy GK amefunguka na kuweka wazi uhusiano wake wa kimapenzi na mwanadada Diva Loveness Love.

Akizungumza na kipindi cha Mkasi kupitia EATV Jumatatu (Jan.12), GK alisema Diva ni mpenzi wake bora kuliko wapenzi wake waliopita, huku akidai kuwa mitandao ya kijamii imechangia ku-boost penzi lao.
 
“inawezekana, kwa sababu ni mwema kwanza halafu na mitandao, unakuta watu wana exchange information, mpenzi wangu wa sasa anazungumziwa sana kwa sababu kuna njia nyingi za kupashana habari” alisema GK.
 
Baada ya kauli hiyo mwanadada Diva ambae ni mtangazaji wa Ala za Roho ndani ya Clouds Fm, kupitia ukurasa wake wa instagram aliandika: “Aww My baby .. My Gk told ya .. I love him so much .. I love his Charm and his intelligence . best Man On earth.. eeh niambieni kasemaje??”

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini