Mume na mke watiwa mbaroni kwa mauaji ya mganga wa jadi


JESHI la Polisi mkoani Kagera linawashikilia watu
tisa kwa tuhuma za mauaji katika matukio mawili
tofauti wakiwemo mume na mke waliomuua
mganga wa jadi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana,
Kamanda wa Polisi mkoani hapa Henry
Mwaibambe, alisema tukio la kwanza lilitokea saa
3:00 usiku wa Januari 14 mwaka huu katika kata
ya Bugarama wilayani Ngara ambapo mganga wa
jadi, Alfaxad John ( 36 ) akiwa anaendesha pikipiki
yake yenye namba za usajili T.237 CDK alikufa
baada ya kupigwa na kitu chenye ncha kali.
Alisema inaaminika mganga huyo alipigwa na
shoka kichwani na kusababisha kichwa
kugawanyika sehemu mbili na shingo
kutenganishwa.
Alisema siku mbili kabla ya tukio hilo la mauaji
John aliibiwa mbuzi watano nyumbani kwake,
aliwaona wezi lakini hakutoka nje ili kulinda
usalama wake.
Baada ya muda alipata ujumbe wa simu ya
mkononi kutoka kwa mpenzi wake ukisema “pole
mpenzi nipo pamoja na wewe ungetoka nje ili
kukabiliana na wezi hao ungeuawa”.
Aliwataja watuhumiwa wanaoshikiliwa kuwa ni
Burhani Tutuleka (40 ) mwalimu wa shule ya
msingi Rwinyana iliyoko kata ya Bugarama na
mkewe Madina Khamisi (35).
Ingawa chanzo cha mauaji hayo bado
hakijajulikana lakini mke wa mtuhumiwa alikuwa
anatibiwa na John na mumewe alikuwa
akimtuhumu mganga huyo kuwa ana uhusiano wa
kimapenzi na mke wake.
Kamanda Mwaibambe alisema tukio la pili lilitokea
saa 8:30 usiku wa Januari 15 mwaka huu ambapo
kundi la wahalifu wasiopungua 10 walimvamia na
kumuua Onesmo Mutta ( 24 ) mkazi wa Mtaa wa
Katotorwansi kata ya Kashai Manispaa ya Bukoba.
Alisema katika tukio hilo wahalifu hao walivamia
nyumba aliyokuwa akiishi Mutta ambayo ilikuwa
na wapangaji wengine na kuanza kuwapiga na
kudai kupatiwa fedha huku wakiwa wamebeba
mapanga na marungu.
Alisema Mutta alichomwa na kitu chenye ncha
kali kifuani upande wa kushoto na kufa papo
hapo. Alisema wapangaji wengine watatu na mke
wa Mutta walijeruhiwa sehemu mbalimbali za miili
yao.
Wahalifu hao walifanikiwa kuiba vitu mbalimbali
vyenye thamani ya Sh 400,000. Aliwataja
waliojeruhiwa kuwa ni Philipina Onesmo mke wa
Mutta ,Edwin Haipolite (23 ) mjasiriamali, Adelene
Simon (27 )n a Denice Gervas

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini