Wastara: Bongo Movie Imeingiliwa na Mapepo, wasanii tupige magoti tusali

Msanii anayefanya vizuri kunako kiwanda cha filamu Bongo, Wastara Juma amefunguka kwamba tasnia ya filamu kwa sasa inaonekana kama imeingiliwa na pepo mbaya kutokana na mambo kwenda ndivyo sivyo kila kukicha.


Akizungumza na Gpl, Wastara alisema tasnia ya filamu imekuwa ni ya migogoro, chuki huku bei ikishuka  jambo ambalo siyo sahihi kwani litawarudisha nyuma wasanii wakati hata kazi hiyo hailipi kihivyo.

 
“Mimi sitengenezi filamu mpaka nielewane na bosi bei kabisa lakini vinginevyo ndiyo maana nimeamua kujikita kwenye biashara ili niweze kuendeleza maisha ya kila siku maana tasnia haieleweki sasa hivi, naona kama pepo mbaya ametuvamia inatakiwa tumuombe Mungu sana,” alisema Wastara.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini