Huyu jamaa ameua watoto wake watano kwa imani za kishirikina candle_light_by_yalco-d4pqdez

candle_light_by_yalco-d4pqdezPolisi wa Pakistan wanamsaka Ali Nawaz Leghari, ambaye ni baba anayekabiliwa  na mashtaka ya kuua watoto wake watano kwa imani za kishirikina.
 
Mama wa watoto hao amesema alikuwa akigombana na mume wake kutokana na kitendo chake cha kujihusisha na masuala ya ushirikina, jaribio la kwanza la kuwawekea sumu watoto wake kwenye chakula cha jioni lilishindwa baada ya mkewe kumshtukia.
Mwanamke huyo alifanikiwa kukimbia na mtoto wake mmoja ambaye ni mkubwa na kuwaacha wengine watano ambao umri wao ni kati ya miaka 15 na wa mwisho miaka 3 ambao aliwapa dawa ya usingizi na kisha kuwanyonga.
Polisi walipofika kwenye nyumba hiyo walikuta miili ya watoto hao Haseena (15), Mukhtiar (12), Shabir (7), Humera (4) na Zameer (3), baada ya kufanya mauaji hayo akichukua basi na kutoroka, huku mtoto aliyenusurika akimwaambia Polisi kuwa baba yake ni muathirika wa dawa za kulevya na alitaka kujihusisha na masuala ya kichawi.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini