WANNE WAFA AJALI YA BASI IRINGA!!!

Muonekano wa lori lenye namba za usajili T122
ALW baada ya kugongana na basi la Fanuel
Express yenye namba za usajili T919 DCD katika
Kijiji cha Ibetelo eneo la Nyororo, wilayani Mufindi
mkoani Iringa.
Basi la Fanuel Express yenye namba za usajili
T919 DCD baada ya ajali hiyo.
ZAIDI ya watu 4 wamefariki dunia na wengine
kadhaa kujeruhiwa baada ya basi la abiria kutoka
Mbeya kwenda Dodoma kugongana na lori katika
Kijiji cha Ibetelo eneo la Nyororo wilayani Mufindi
mkoani Iringa.
Kamanda wa Polisi Mkoani Iringa, Ramadhani
Mungi amesema kuwa ajali hiyo imetokea saa
4.45 asubuhi na kuhusisha basi mali ya Kampuni
ya Fanuel Express yenye namba za usajili T919
DCD kugongana uso kwa uso na lori lenye namba
za usajili T122 ALW mali ya Kampuni ya
Transisco lililokuwa likitokea Dar es Salaam
kwenda nchi jirani.
Amesema watu wawili waliokuwa ndani ya basi
wamefariki papo hapo na wote waliokuwa ndani
ya lori wanahofiwa kufa, ambapo hadi kufikia saa
7 mchana, watu wawili ndani ya lori walikuwa
wamethibitika kufariki dunia na kufanya waliokufa
kuwa wanne.
Zoezi la kuondoa miili iliyokuwa ndani ya lori
linaendelea ambapo amesema kuwa huenda idadi
hiyo ya waliokufa ikaongezeka.
Akielezea mazingira ya ajali hiyo, Kamanda Mungi
amesema kuwa basi hilo lilikuwa likijaribu kulipita
basi lililokuwa mbele yake katika eneo ambapo
palikuwa na lori lingine lililoharibika, wakati huo
huo lori lililohusika katika ajali hiyo lilikuwa
likikwepa lori lililoharibika pamoja na basi hilo,
ndipo magari hayo yalipogongana uso kwa uso
katika jitihada za kukwepana.
Majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika
Hospitali ya Mafinga, Iringa.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini