WANAFUNZI 459 WA DARASA LA KWANZA WANASOMEA KWENYE DARASA MOJA JIJINI DAR

bbbdKatika hali isiyo ya kawaida, zaidi ya wanafunzi 459 wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Saku iliyopo Chamazi, Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, wanasoma katika darasa moja.
Hali hiyo ya wanafunzi kusoma katika darasa moja na wengine chini ya miti inayozunguka shule hiyo, inachangiwa na upungufu wa majengo ya shule hiyo ambayo ina vyumba saba vya madarasa huku ikiwa na zaidi ya wanafunzi 2,038.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Saku, Salome Munisi alisema shule yake inakabiliwa na changamoto kubwa ya uchache wa madarasa pamoja na wingi wa wanafunzi kuliko uwezo wa vyumba vya madarasa walivyonavyo.
Munisi alisema idadi ya wanafunzi walioandikishwa darasa la kwanza mwaka huu ni kubwa kuliko darasa la pili ambalo lina wanafunzi 436, wakiwamo wanaume 217 na wasichana 219.
Kipindi cha mitihani inabidi wanafunzi wafanye mtihani chini ya mti kwa sababu wako wengi darasani, huwezi mwalimu kuwapa mtihani watatizamiana na itakuwa ngumu kupima kiwango cha elimu kwa wanafunzi kwa sababu watajaza majibu yote yanayofanana“:Munisi.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini