Simba yatinga nusu Fainali ya Mapinduzi


Vijana wa timu ya Simba yenye makao yake makuu Msimbazi jijini Dar es Salaam
katika michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar, timu ya Simba imetinga hatua ya nusu fainali baada ya kuichakaza Taifa Jang'ombe mabao 4-0 katika mchezo wa robo fainali uliochezwa jana usiku mjini Zanzibar. Michezo mingine ya robo fainali inaendelea leo kwa timu za KCC ya Uganda kumenyana na Polisi Zanzibar, Azam ya Tanzania itakwaruzana na Mtibwa Sugar pia ya Tanzania, huku Yanga ikikamilisha michezo ya hatua hiyo kwa kupambana na JKU ya Zanzibar saa mbili usiku mjini Zanzibar.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini