Dogo Janja: Naogopa kumwanika mpenzi wangu kwenye mitandao!

Rapper wa Tip Top Connection, Dogo Janja amesema yeye ni miongoni mwa watu ambao hawawezi kuwaweka wazi wapenzi wao kwenye mitandao.
11376111_1621732448079693_614238344_n (1)
Dogo Janja ameiambia Bongo5 kuwa kitu anachoogopa ni kuanza kutupiana maneno wakati wanapoachana.
“Unajua mapenzi ya kwenye mitandao ukigombana tu na mpenzi wako au mkikosana, watu wataanza kutupiana maneno ingawa kwa watu wengine haitokei,” amesema. “Pia unajua kila mtu kalelewa tofauti na mimi sio kwamba sina girlfriend, mimi naamini katika sanaa yangu watu wamenijua mimi kama mimi. Ningependa watu waendelee kumjua Dogo Janja. Sometimes vitu kama hivi vinaweza kukupotezea uaminifu wako, unajua kuna watu wanatuangalia,” ameongeza rapper huyo.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini