MAGUFULI Aahidi Tanzania Mpya Kama Atachaguliwa!

Magufuli Akifanya Kampeni Mbeya 
Mgombea wa Urais kupitia CCM, Dk John Pombe Magufuli amemaliza kampeni katika mkoa wa Njombe na kuwaomba Watanzania kumchagua kwa kuwa ana mpango wa kuijenga Tanzania mpya.

Dk Magufuli aliwaambia wakazi wa kijiji cha Mlangali wilayani Ludewa kuwa serikali za awamu nne zilizopita zilifanya makubwa kwa kuboresha mazingira ya maendeleo hivyo awamu yake itakuwa ni ya kukamilisha mabadiliko.

"Awamu ya kwanza ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere ndiyo iliyoleta Uhuru kutoka kwa wakoloni na ukombozi wa kweli kwa kuunganisha makabila zaidi ya 121.

"Awamu za Mzee Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Rais Jakaya Kikwete hizi nazo zimefanya makubwa kwa kuendelea kutuweka pamoja kwa amani bila kupigana na kujenga barabara kama hizi japo za vumbi lakini zinapitika, " alisema Dk Magufuli.

Alisema kutokana na mafanikio ya Serikali zilizopita, awamu ya tano itakuwa ni ya maendeleo ya barabara, umeme, viwanda, elimu, maji, afya, ajira na kuboresha mazingira ya wafanyakazi na wakulima.

Kauli ya mgombea huyo inakuja siku moja baada ya mgombea wa Urais wa Chadema kupitia mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa kuahidi juzi kuwa iwapo atapitishwa, Serikali yake itakuwa ni ya mabadiliko na ukombozi.
Dk Magufuli alisema atakuwa rais wa Watanzania wa dini na vyama vyote.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …