Petit Man Amuanika Mrithi wa Dada wa DIAMOND, Esma!

petit-na-kifaa-esmaImelda Mtema
Mpambe wa staa wa Filamu Bongo, Wema Sepetu, Hamadi Manungwa ‘Petit Man’, juzikati alimuanika rasmi mrithi wa aliyekuwa mkewe, Esma Abdul ‘Esma Platnumz’ baada ya hivi karibuni kuingia kwenye mgogoro wa ndoa.
Baada ya gazeti hili kuanika habari ya kuvunjika kwa ndoa hiyo wiki iliyopita huku Wema akitajwa kuwa chanzo ambapo yalizuka mambo mengi mpaka watu kupelekana polisi, hivi karibuni Petit Man alimuanika mwanamke mwingine akidai ndiye wa kuchukua nafasi ya Esma.
esmaBaada ya picha hizo kuzagaa mtandaoni, mwandishi wetu alizungumza na Petit Man ambaye alisema: “Niko kwenye mchakato wa kutoa talaka kwa vile sipendi kuwekwa kwenye mitandao na kudhalilishwa kila wakati, baada ya talaka nitaoa haraka.”
Esma kwa upande wake alisema anachosubiri ni talaka yake tu kwani ameshachukua baadhi ya vitu vyake kwenye nyumba waliyokuwa wakiishi na Petit Man.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini