Msanii Bongo Movie Adaiwa Kufumaniwa na Kushushiwa Kichapo Heavy!

Utata! Msanii wa Bongo Movies, Gidion Simon ‘Kabraza’ aliyewahi kushiriki katika Sinema za Nimeshindwa, Mkuki kwa Nguruwe na zinginezo anadaiwa kufumaniwa lakini ameibuka na kukanusha vikali tuhuma hizo baada ya kusambaa kwa picha yake kwenye mitandao akiwa amevimba uso.
 Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Kabraza ambaye amewahi kushirikiana na wasanii wa vichekesho kama Kinyambe, Senga na Matumaini alisema madai kuwa amefumaniwa hayana ukweli na kwamba kuvimba kwake kunatokana na kuugua jipu.
 “Sikufumaniwa, ninaumwa jipu eneo la paji la uso, limenisababishia maumivu makali na kuvimba uso mzima, naumia sana, watu wanaozusha maneno yasiyo na ukweli,” alisema Kabraza.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini