Elewa sababu KUU zinazomfanya mwanamke asipate mimba -3

Mpenzi msomaji, naendelea kuelezea sababu zinazomfanya mwanamke kushindwa kupata ujauzito na namna ya kutumia kalenda kujua siku za kupata ujauzito.
 Kalenda ya Ovulation au kalenda ya kubeba mimba ni mzunguko wa mwezi baada ya kupata hedhi yaani siku ya kwanza unayopata damu yako ya hedhi hadi siku kabla ya kupata tena hedhi nyingine.
 Ili kujua mzunguko huo vyema, inatubidi tuchunguze hedhi yetu kwa miezi isiyopungua sita. Lakini kama una haraka na huwezi kuchunguza kwa miezi sita, chunguza kwa miezi mitatu.
 Unaweza kufanya hivyo kwa kutumia kalenda ya kawaida na kwa kuziwekea mduara kwa kalamu siku zako za mwezi, yaani siku ya kwanza ya kupata damu ya hedhi hadi siku ya mwisho kabla ya hedhi inayofuata. Mzunguko wako wa mwezi ni siku ya kwanza ya hedhi hadi siku ya kabla ya kuanza hedhi nyingine.
 Kwa mfano, iwapo umepata siku Julai 2 na ukapata tena tena Julai 29, mzunguko wako ni wa siku 28. Kwa kawaida mzunguko wa siku 28 ndiyo mzunguko wa kawaida kwa wanawake wengi.
Lakini kuna baadhi ya wanawake huwa na mzunguko wao chini ya siku 28 na wengine huwa na mzunguko wa hadi siku 35.

 Wakati wa Ovulation katika mzunguko wa mwezi huainishwa na lateal phase, katika mzunguko wako. Unaweza kujua muda wa Ovulation katika mzunguko wako wa mwezi kwa kutoa idadi ya siku za luteal phase.
 Katika kuhesabu huko, utapata mzunguko mfupi na mrefu. Chukua mzunguko mfupi wa mwezi na hesabu idadi ya siku katika mzunguko huo. Toa 18 katika mzunguko huo na utapata idadi fulani.
Halafu anza kuhesabu siku yako ya kwanza ya mzunguko wa hedhi katika mwezi unaofuata kwenda mbele hadi kufikia namba uliyopata, hivyo utaweza kupata siku ambayo una uwezekano mkubwa wa kubeba mimba.

 Kwa mfano, mzunguko wako mfupi ni siku 29, unatoa 18 katika 29 na unapata 11. Iwapo siku yako ya kuanza hedhi mwezi ujao ni Oktoba 3, ongeza siku 11 kuanzia siku hiyo. Hivyo siku ambayo una uwezekano mkubwa wa kubeba mimba itakuwa Oktoba 14.
 Halafu chunguza idadi ya siku za mzunguko wako mrefu wa hedhi. Toa siku 11 kutoka katika idadi ya siku za mzunguko huo na utapata namba fulani.
 Halafu tena anza kuhesabu katika mzunguko wako ujao wa hedhi kwenda mbele hadi kufikia siku ambayo una uwezekano wa kupata mimba. Kwa mfano, iwapo mzunguko wako mrefu ni siku 31, toa 11 katika mzunguko huo na utapata 20.
 taendelea wiki ijayo.
uwezekano mkubwa wa kubeba mimba au Ovulation window kitabibu.
Ovation huweza kubadilika kidogo katika mzunguko wako wa hedhi kwa sababu Ovulation huweza kucheleweshwa na sababu mbalimbali kama vile wasiwasi au fikra nyingi, ugonjwa, lishe au kufanya mazoezi.

 Kipindi cha Ovulation kinaainisha siku za kubeba mimba? Kipindi cha kubeba mimba huanza siku 4 hadi 5 kabla ya Ovulation na humalizika saa 24 hadi 48. Hii ni kwa sababu muda wa Ovulation huweza kuchelewa au kuwahi kutokana na sababu mbalimbali.
 Pia kwa sababu mbegu ya kiume huwa na uhai kwa siku 4 hadi 5 na yai huweza kuishi kwa saa 24 hadi 48 baada ya kuingia katika tumbo la uzazi.
Hivyo kwa kujua siku hizo humsaidia mwanamke kufahamu kipindi chake cha Ovulation kimewadia hivyo kuweza kukutana na mumewe au mwenza wake wakati huo ili aweze kubeba mimba.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini