UKAWA WAMVURUGA MREMA WA TLP, AJIBU MAPIGO KIHIVI...

Na Safina Sarwatt, Moshi 
MWENYEKITI wa Chama Cha Tanzania Labour Party (TLP), Agustine Mrema, amesema mgombea urais wa Ukawa kupitia Chadema, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa hana ubavu wa kushinda katika kinyang’anyiro cha Uchaguzi Mkuu Oktoba 25 mwaka huu.

Alisema mgombea huyo kupitia Ukawa hawezi kushinda nafasi hiyo kwa kuwa hana uzoefu na siasa za upinzani na ni CCM “B”.

Mrema aliyasema hayo jana katika ufunguzi wa kampeni ya mgombea urais wa TLP, Maximillan Lyimo, iliyofanyika katika viwanja vya njia panda ya mji mdogo wa Himo Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro.

Mrema ambaye aliwahi kugombea urais mwaka 1995 kupitia chama cha NCCR Mageuzi, alisema anashangazwa na maneno yanayoenezwa na Ukawa kwamba yeye ni CCM wakati wao wamemchukua mgombea wa urais kutoka chama hicho tawala.

“Ukawa wanaita mimi CCM B’wananichafua kwa wananchi wangu na kama mimi ni CCM mbona nimekaa upinzani kwa zaidi ya miaka 20 na mgombea wao aliyetoka CCM hajakaa hata mwezi aitweje? Basi na mgombea wao ni CCM” B’,”alisema Mrema.

Hata hivyo Mrema alieleza sababu za yeye kutoungana na vyama hivyo vinne vinavyounda Ukawa akisema umoja huo hauna msaada wowote kwa wananchi bali ni wa maslahi ya mtu mmoja na chama chake.
Pia Mrema alitumia mkutano huo kuiponda Chadema kwamba siyo ile ya zamani bali imetekwa na CCM.

“Niwaambie kwamba mimi ni mpizani wa kweli ndiyo maana nimebaki na chama changu sijaburuzwa na mtu, tuna msimamo leo hii ningekuwa mgeni wanani kama ningejiunga na Ukawa ninyi wenyewe ni mashahidi maprofesa wamekimbia, yuko wapi Dk. Slaa?” aliuliza Mrema.

Naye Katibu Mkuu wa TLP, Nancy Mrikario,aliwataka wanawake kutokudanganywa na baadhi ya wanasiasa wasiokuwa na nia njema kwa kuwarubuni na kuwahonga vitenge na fulana.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini