ELEWA UNDANI WA UGONJWA WA KIFUA KIKUU (TB)-2




Naendelea kuelezea undani wa ugonjwa wa kifua kikuu ambapo leo nitazitaja dalili zake.

Dalili za kifua kikuu hutegemea sana ni mahali gani bakteria wa TB wanakuaw. Kwa kawaida bakteria wa kifua kikuu wanakuwa kwenye mapafu na kusababisha kifua kikuu cha mapafu. 
Kifua kikuu cha mapafu kinaweza kusababisha kifua kikali kinachochukua zaidi ya wiki tatu, maumivu ya kifuani na kukohoa damu au makohozi.

Dalili nyingine za ugonjwa wa TB ni pamoja na udhaifu au uchovu, kupungua uzito, kukosa hamu ya kula, baridi, homa na kutoka jasho usiku. Kifua kikuu tuli hakina dalili.

TIBA 

Kwa kawaida, mgonjwa wa kifua kikuu anatumia vidonge kila siku wakati wa matibabu yanayosimamiwa.
Ugonjwa wa kifua kikuu kikali unaweza kutibiwa kwa mchanganyiko wa antibiotics. Mchanganyiko sahihi wa dawa za kifua kikuu hutoa kinga na tiba.

Tiba inayofaa humwezesha haraka mgonjwa wa kifua kikuu kutoambukiza na kwa hiyo huzuia kuenea zaidi kwa kifua kikuu. Kufanikisha tiba ya TB, huchukua miezi sita hadi minane ya matumizi ya dawa ya kila siku.
Dawa za aina mbalimbali zinatakiwa kutibu kifua kikuu kikali. Kutumia dawa mbalimbali kufanya kazi nzuri ya kuua bakteria wote na huenda ikakinga dhidi ya usugu kwa dawa.

Dawa zinazotumika zaidi ni Isoniazid, Rifampin (Rifadin, Rimactane), Ethambutol (Myambutol) na Pyrazinamide.
Kuhakikisha matibabu kamili, mara nyingi inapendekezwa kuwa mgonjwa ameze vidonge mbele ya mtu atakayesimamia matibabu. Njia hii inajulikana kuwa DOTS (matibabu yanayofuatiliwa moja kwa moja, muda mfupi). DOTS hutibu kifua kikuu kwa 95% ya wagonjwa.

KINGA

Dawa inayoitwa Isoniazid (INH) inaweza kutumiwa kama kinga kwa wale walio hatarini zaidi kuambukizwa kifua kikuu au kwa wale wenye kifua kikuu tulivu. 
Itaendelea wiki ijayo kwenye gazeti hilihili.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini