Posts

Showing posts from September, 2015

INATISHA SANA! Watu Watano wa Familia Moja Wachinjwa Kama Kuku Mkoani Simiyu

Image
Watu watano wamefariki dunia papo hapo kwa kukatwa katwa mapanga na kuchinjwa kama wanyama katika kitongoji cha Kisesa kata ya Bugalama wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu. Watu hao ambao ni wa familia moja walifanyiwa unyama huo kwa kukatwa katwa mapanga sehemu ya shingoni. Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa polisi Mkoani hapa Gemine Mushy alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 9 ambapo Baba, Mama pamoja na watoto wao 3 waliuawa. Mushy aliwataja waliofanyiwa unyama huo kuwa George Charles (30) ambaye ni Baba wa familia, Siku John (23) Mama wa Familia na watoto wao ambao ni Mchambi George (7) Tuma George (5) pamoja na Amos George (Miezi 9) wote wasukuma wa kitongoji hicho. Kamanda Mushy alieleza chanzo kuwa ni mgogoro wa ardhi kati ya marehemu (George) pamoja na Baba yake wa kambo ambaye alinunua kipande cha ardhi alikokuwa akiishi marehemu. Aliongeza kuwa baada ya tukio hilo jeshi la polisi lilifanya msako na kuwakamata watuhumiwa 3 ambao aliwataja kuwa ni Miga

MAGUFULI: Nakerwa na Vigezo vya Uzoefu Kuomba Ajira

Image
Mgombea wa urais kupitia CCM, Dk John Magufuli amesema iwapo atapewa ridhaa ya kuingia Ikulu atapambana kuhakikisha Watanzania wengi wanapata ajira na kwamba anakerwa sana na kigezo cha mtu kuwa na uzoefu ndio apatiwe ajira. Dk Magufuli alienda mbali na kusema kuwa kama kuna uwezekano, kipengele hicho kinachowataka watu kuwa na uzoefu wa miaka kadhaa kama kigezo cha kuajiriwa huku akitoa mifano ya watu wanaaomba nafasi mbalimbali za uongozi wa kisiasa akiwepo yeye mwenyewe kuwa hawana uzoefu wa nafasi hizo lakini wana uwezo wa kuongoza. Katika kampeni zake mjini Iringa, Magufuli pia aliahidi kuwa serikali yake itajikita katika ujenzi wa viwanda mjini humo ili kupunguza tatizo la ajira kwa vijana. Alisema kuwa wapo vijana wengi wanaohangaika kupata ajira baada ya kuhitimu kwa kuwa ajira nyingi zinahitaji watu wenye uzoefu wa kufanya kazi hivyo inakuwa kikwazo kikubwa kwa wahitimu kupata nafasi hizo. ‘’Vijana wengi wanaomaliza vyuo mbalimbali wanapatashida kupata ajira kutokana

Polisi Arusha Wasambaratisha Utafiti wa Nani Mkali kati ya LOWASSA na MAGUFULI Uliokuwa Ukifanywa Mitaani!

Image
Wakati tafiti za kienyeji zenye lengo la kupima kukubalika kwa wagombea urais, hasa Dk John Magufuli na Edward Lowassa zikizidi kuongezeka, polisi jijini Arusha mwishoni mwa wiki walitumia nguvu kutawanya vijana waliokuwa wakiendesha kura za maoni kwenye stendi ndogo ya mabasi na soko kuu. Tangu kutangazwa kwa matokeo ya utafiti uliofanywa na taasisi za Twaweza na Ipsos, vijana kwenye maeneo mbalimbali yenye mikusanyiko, hasa sokoni na kwenye baa wamekuwa wakiendesha tafiti zao za kienyeji wakiwa na lengo la kuonyesha hali halisi ilivyo mitaani tofauti na matokeo ya tafiti hizo mbili. Katika tafiti hizo za Ipsos na Twaweza, Dk Magufuli, ambaye anagombea urais kwa tiketi ya CCM, alikuwa mbele ya Lowassa anayegombea kwa tiketi ya Chadema na vyama vinavyounga mkono Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), lakini matokeo hayo yamepingwa vikali na wadau mbalimbali, huku yakiamsha tafiti za kienyeji mitaani. Katika tukio lililotokea mjini Arusha, vijana walikuwa wakiendesha utafiti wao

Je, Kweli Jeshi la Magereza TZ Limetangaza Ajira Mpya?! Jibu La Kamishna Lipo Hapa...

Image
Katika siku za hivi karibuni, kumekuwepo na tangazo kuhusu nafasi za ajira katika Jeshi la Magereza linalodaiwa kuwa limetolewa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza na kusambazwa kwenye baadhi ya Mitandao ya kijamii. Umma unajulishwa kuwa taarifa hizo siyo za kweli.  Jeshi la Magereza linapenda kuufahamisha umma kuwa ajira hutolewa na kutangazwa kupitia Vyombo vya Habari pamoja na tovuti ya Jeshi la Magereza ya www.magereza.go.tz  na si vinginevyo. Hivyo, Jeshi la Magereza linawatahadharisha Wananchi wote kuwa macho na mitandao ya kitapeli inayotoa taarifa za kupotosha na kuleta usumbufu mkubwa kwani mfumo wa ajira ndani ya Jeshi la Magereza ni wa wazi na unafuata Kanuni na Taratibu za ajira za Utumishi wa Umma.  Imetolewa na kusainiwa na,  John C. Minja  KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA  29 Septemba, 2015

Roma Adai Hajapata Barua ya Wimbo Wake Kufungiwa....Awapa Ushauri BASATA

Image
Siku chache baada ya Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kutoa tamko la kuufungia wimbo wa Roma ‘Viva’, rapa huyo amesema kuwa bado hajapata barua rasmi ya Baraza hilo. Amesema yeye pia ameiona habari hiyo kwenye mitandao na sababu zilizoainishwa na Baraza hilo kuifungia ‘Viva’. Licha ya kukiri kuwa hafahamu taratibu zinazotumiwa na Baraza hilo kutoa taarifa kama hizo, Roma alilishauri Baraza hilo kuweka utaratibu wa kuzisikiliza nyimbo kabla hazijatoka ili kuepusha usumbufu. "Nisiwe muongo, sijui taratibu wanazotumia kufikisha taarifa zao.Mi nadhani ingekuwa rahisi kama artist hajaachia nyimbo yake mpya ama hajafanya kazi yake ya sanaa,iwe inawasilishwa katika hicho chombo.Nadhani hapo tungekuwa tunaenda sawa," amesema Roma. Hata hivyo,Afisa habari wa BASATA,Artistide Kwizela amefafanua taratibu zinazotumiwa na baraza hilo kufikisha ujumbe kwa umma pale wanapoifungia kazi fulani ya msanii. "Kuna kufungiwa kwa maana ya msanii mwenyewe kuandikiwa,lakini kama kuna

LOWASSA Akerwa Wafuasi wake Kupigwa Mabomu!

Image
Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa ameeleza kusikitishwa na kitendo cha polisi kuwapiga mabomu wananchi wa Tanga waliokuwa wakitoka kwenye mkutano wake. Lowassa alisema hayo jana kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Korogwe baada ya juzi kulazimika kuvunja mkutano wake kutokana na wingi wa watu na kusababisha wananchi wengi kuzimia mjini Tanga. Baada ya kuvunja mkutano huo, polisi walipiga watu mabomu ili kuwatawanya jambo ambalo Lowassa alisema limemsikitisha na kuwaomba waache kufanya hivyo na badala yake watoe ushirikiano kwa wananchi. “Nasikitika polisi kupiga mabomu. Tushirikiane katika jambo hili ili kuondoa vurugu,” alisema Lowassa huku akiwashukuru wananchi wa Tanga kwa mapokezi makubwa aliyoyapata. Lowassa, ambaye jana alifanya mikutano ya aina yake akielekea Dar es Salaam kwa gari, alisimamishwa na umati mkubwa wa watu waliokuwa wametanda barabarani katika Jimbo la Muheza na kuhutubia akiwa juu ya gari akisema anahitaji kura za kutosha ili aweze kuleta m

LOWASSA Aipasua CCM

Image
Lowassa Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Moshi Mjini, Zakaria Laizer amepewa likizo ya lazima ya siku 30, akituhumiwa kumuunga mkono mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa. Kiini cha kupewa likizo hiyo kinatokana na kukutwa akipata chakula na viongozi wawili wa zamani wa CCM katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha, ambao sasa wamehamia Chadema. Viongozi hao ni katibu wa zamani wa Itikadi na Uenezi wa mkoa wa Arusha, Issack Kapriano maarufu Kadogoo na Katibu wa zamani wa Uchumi na Fedha mkoa Kilimanjaro, Paul Matemu. Katibu wa CCM Wilaya ya Moshi, Loti Ole Nesele ametithibitishia jana kuwa Laizer kapewa likizo hadi baada ya uchaguzi. “Miye sipo Moshi niko Babati, lakini ni kweli alipewa barua hiyo ya likizo wiki iliyopita, ukiniuliza sababu sitakwambia kwa sababu ni siri za mtumishi na ofisi,” alisema. Hata hivyo, chanzo cha habari cha uhakika kinasema, Kadogoo ambaye ana undugu na Laizer alimpigia simu ndugu yake huyo akimjulisha kuwa angepita Moshi akienda Mwanga, hivyo amsaid

MAGAZETI YOTE YA LEO ALHAMISI TAREHE 1/10/2015...SIASA, UDAKU, MICHEZO NA BURUDANI

Image
Kutoka Dar es Salaam Tanzania leo Alhamisi Octoba 1, 2015 tayari nimeyakusanya Magazeti yote na stori zake kubwakubwa kukusogezea hapa, headlines baada ya headlines kwenye Magazeti ya Udaku, Michezo na Hardnews, zote ziko hapa  . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

PICHAZ: SHUHUDIA MAMA SAMIA AKIPIGA KAMPENI SIRARI MKOANI MARA LEO

Image
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Musoma, kuendelea na ziara za mikutano ya kampeni katika mkoa wa Mara leo. Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akifurahia Mcheza Ngoma alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Musoma, kuendelea na ziara za mikutano ya kampeni katika mkoa wa Mara leo. Mgomea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mgombea Ubunge jimbo la Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Musoma, kuendelea na ziara za mikutano ya kampeni katika mkoa wa Mara leo.   Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, akiwanadi wagombea Ubunge, wa majimbo ya Tarime, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo Sirari mkoani Mara. Kulia ni Chrisopher Kangoye (Tarime Vijijini) na kushoto ni Michael Kimbaki (Tarime Mjini).   Wananchi wakimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiket