HESHIMA NI UWEZO WAKO WA FARAGHA

Mdau wa kona hii, mada ya wiki hii inazungumzia heshima ya mtu kwa mpenzi wake ni uwezo wake wa kumdhibiti mwenza wake wanapokuwa faragha. Kwa maana nyingine namaanisha kuteka hisia za mpenzi wako mnapokuwa kwenye dimbwi la mahaba.
Mapenzi ni utundu
Mapenzi yanahitaji ubunifu na utundu wa hali ya juu sana kwani sehemu kubwa ya heshima ya mwanadamu kwa mwenza wake inapatikana wakati wa faragha.
Mapenzi usahaulisha shida
Inawezekana ukawa huna pesa za kutosha lakini ukifika faragha mpenzi wako anafurahi na kusahau kama kuna shida, anasahau kama alipaswa ale kwanza ndiyo mkutane lakini mlijikuta mkiingia ulingoni bila kula na hamkuliona hilo kwa sababu ya hisia kali za mapenzi zilizowakabili.
Machungu hugeuka furaha
Wahusika hujikuta wakihama kutoka ulimwengu wa kawaida na kuwa ulimwengu mwingine wa raha, kama walikuwa ulimwengu wa kimaskini basi hujihisi wako paradiso, kama walikuwa kwenye machungu basi hugeuka na kuwa wenye furaha.
Faragha ndipo penye heshima
Kama ulikuwa hujui heshima yako ni uwezo wa wewe uwapo faragha na mpenzi wako kwa kutawala mchezo wenu sambamba na kumfikisha kwenye kilele cha mlima.
Ustaa faragha hauna maana
Unaweza ukawa staa, maarufu na muonekano mzuri sana wa nje, kila mtu anayekuona anakubali utanashati au urembo wako, lakini kumbe katika sita kwa sita si lolote si chochote, hujitumi, hujui namna ya kumfanya mwenza wako afurahie mwisho wa safari yake.
Pesa si chochote
Si kweli kwamba pesa zako zinaweza kununua penzi la kweli, lakini ujuzi wako unaweza kuongeza heshima juu ya pesa zako.
Ukiwa goigoi pesa zako si kitu kwani kama ni mwanamke utasikia analalamika; “wewe nani alikuambia kwako nimefuata kula, kulala na kuvaa, kama kitanda si hata kwetu kipo, kama kula kwetu kuna vyakula kibao, sikuja hapa kufuata pesa zako nimefuata penzi lako.”
Elimu
Faragha aihitaji uwezo wa kufanya hesabu za magazijuto, kwa hiyo kama ukijifanya una elimu mpaka eneo hili nyeti basi ujue umefeli, elimu yako haisadii kitu kama huna uwezo wa kumtawala mwenza wako.
Mjanja
Haijalishi ujanja wako wa mjini, kama huwezi mambo unapokuwa jukwaani heshima yako hutoweka.
Nakaribisha maoni yenu kuhusiana na mada hii ambayo yatatoka katika toleo lijalo, pia usikose kutembelea ukurasa wetu wa Mimi Na Uhusiano kwenye Mtandao wa Facebook ili ujifunze mengi kuhusu mapenzi.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini