CCM Wamtimua Mwandishi wa MWANANCHI Katika Kampeni za MAGUFULI Baada ya Kuripoti Zomea Zomea ya Mbeya!

Mwandishi wa gazeti la MWANANCHI ndugu Peter Elias ametimuliwa kutoka msafara wa kampeni za mgombea urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ndugu John Magufuli, imethibitishwa.
Mwandishi huyo ametimuliwa kwa kosa la kuripoti tukio la mgombea huyo kuzomewa na wafuasi wa Chadema jijini Mbeya hivi karibuni kinyume cha
makubaliano.
Mwandishi huyo aliripoti katika gazeti hilo kwa kichwa cha habari "Magufuli akabiliana na UKAWA Mbeya" na kuweka picha ya mgombea huyo akionyeshwa alama ya vidole viwili.

Source: US

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini