MAGUFULI Atetea Safari za Nje za Rais

magufuli akiongea na wakazi wa kijiji cha Pawaga

Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM, Dk. John Magufuli.
Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM, Dk. John Magufuli,  amewashangaa watu wanaokejeli safari za nje za Rais Jakaya Kikwete, akisema manufaa ya ziara hizo ni makubwa kuliko wanavyofikiri.
Amesema kupitia safari hizo, Rais Kikwete amefanikiwa kuwashawishi wafadhili kutoa misaada ya miradi mbalimbali nchini. 

Aliyasema hayo kwenye mkutano wa kampeni katika kata ya Mvumi Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma jana.
Dk. Magufuli alitoa mfano wa Sh. bilioni 992 zilizotolewa na Serikali ya Marekani hivi karibuni kupitia mfuko wa MCC kwa ajili ya miradi ya umeme kama sehemu ya matunda ya safari za Rais Kikwete nchi za nje.
“Mabilioni yaliyotolewa na MCC, yatasaidia kusambaza umeme katika mikoa na vijiji vingi nchini na tayari mipango imekamilika ya kuwafikishia wananchi nishati hiyo,” alisema. 

Wakati huo huo, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimelaani kitendo kinachodaiwa kufanywa na wafuasi wa Ukawa kuvamia ofisi za chama hicho mkoani Tanga na kufanya mashambulizi mbalimbali.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mjumbe wa Kamati ya Kampeni za CCM, January Makamba, shambulio hilo lilifanywa juzi kabla na baada ya Ukawa kumaliza mkutano wa kampeni katika uwanja wa Tangamano kwa kurusha chupa zenye haja ndogo. 

Aidha, alidai kuwa tukio hilo lilifuatiwa na la mgombea wao wa urais, Dk. John Magufuli, la kusimamishwa njiani na vijana wa Ukawa pamoja na kupiga kelele kwenye mkutano wake wa hadhara mkoani Mbeya kuwafanya wananchi wasimsikilize.
CHANZO: NIPASHE

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini