Wanaotukana MATUSI Kwa Wanasiasa Wapewa za Uso!

Dully Sykes amedai kuwa hafungamani na upande wowote wa chama cha siasa na amewataka watu kuacha kukashifu viongozi wanaogombea nafasi za uongozi.
Dully
Akizungumza na 255 ya XXL ndani ya Clouds FM, Dully aliwakumbusha watu kujua kuwa kuna maisha baada ya uchaguzi.
“Mimi ni binadamu kama binadamu wengine na mimi ni mwananchi kama wananchi wengine, lakini mimi Mungu alinipa kipaji cha kuwa kioo cha jamii.
Kama nimepewa kipaji cha kioo cha jamii naamini naweza kuongea kitu. Mimi sipo chama chochote na ninapoona mtu anamkebehi mtu mzima na kumwambia vitu ambavyo kiukweli kabisa vinaweza vikamuumiza mwingine. Kwa mfano wewe mvae mgombea halafu angalia post mbaya za watu jinsi zinavyokukabili. Hiyo imekuwa haipendezi, mimi nimeona watu jinsi wanavyowazungumzia vibaya viongozi. Kumbuka kuna maisha baada ya uchaguzi,” alisisitiza Dully Sykes.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini