MBINU CHAFU ZA CCM UCHAGUZI MKUU 2015...UKAWA WASHTUKA!

 Serikali imetakiwa kutokujihusisha na mpango wowote wa kutaka kuvuruga zoezi la uchaguzi mkuu kwa kutumia vyombo vya ulinzi na usalama kwani kufanya hivyo ni hatari na kunaweza kuvuruga amani ya nchi.

Akihutubia maelfu ya wakazi wa jimbo la Vunjo mwenyekiti wa Chadema taifa, Freeman Mbowe ameonyesha kusikitishwa kwake na kile kinachodaiwa ni mbinu chafu zinazofanywa na CCM za kutaka kuvuruga uchgauzi mkuu kwa kujaribu kuvuruga utendaji wa tume ya taifa ya uchgauzi.
Aidha Freeman Mbowe ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa UKAWA ameitaka serikali kujibu tuhuma za kuweka maafisa wa vyombo vya usalama ndani ya tumeya taifa ya uchaguzi huku pia akigusia mbinu chafu za kura katika baadhi ya maeneo.

Akiwa mjini Vunjo Edward Lowassa amehutubia mikutano ya hadhara katika maeneo ya Kahe, Kirua na Himo ambapo amewataka watanzania kuhakikisha wanampigia kura nyingi tena za kishindo na kwamba serikali atakayoiunda itajikita katika kusimamia rasilimali za nchi.

Akihutubia katika ufunguzi wa kampeni za ubunge ndani ya jimbo la Vunjo na huku akionekana dhahiri kuwa na nafasi kubwa ya kuibuka mshindi kwa kiti cha ubunge ndani ya jimbo hilo James Mbatia pamoja na masuala mengine amewahakikishia wana-Vunjo kuwaletea maendeleo waliyoyakosa kwa miaka mingi iliyopita.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini