KATIBU WA CCM ITIKADI NA UENEZI NAPE NAUYE AMPA MANENO MAZITO MH EDWARD LOWASSA

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amewaomba wananchi kumuombea dua njema mgombea urais wa Ukawa, Edward Lowassa ili Oktoba 25 ashuhudia ushindi wanaoupata CCM.

Nnauye alisema hayo juzi, mjini Morogoro wakati akizindua safari ya ‘Nimeshtuka’ ambayo inawahusisha wasanii mbalimbali ambao awali walikuwa wanachama wa Chadema wakimuunga mkono Lowassa kabla hawajarudi CCM.

Alisema kuwa chama chake kitaibuka na ushindi wa kishindo na kwamba, itakuwa vizuri kwa mgombea huyo kushuhudia matokeo yakitangazwa akiwa na afya njema.

Akizungumzia wapinzani, alisema anapenda upinzani wa vyama vya siasa kwa kuwa wamekuwa wakiishtua Serikali ya CCM kwenye mambo machache ambayo yamekuwa yakilala au kwenda kinyume na utaratibu.
“Katibu wetu Kinana (Abdurahman) anatushtua kwa kuwa sisi sio kwanza tunapatia kila kitu kwa asilimia 100, lakini baadhi ya mambo machache tunayarekebisha kupitia wapinzani,” alisema Nape.
Nape alisema Lowassa alipokwenda Ukawa alidhani amepata, kumbe amepatikana na kusema kuwa CCM imejipanga na imejiandaa kushinda uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka huu kwa kuwa Watanzania wengi wana imani na utendaji wa mgombea wao wa urais, Dk John Magufuli.

Kwa upande wake, kiongozi wa wasanii hao ambao wamejitoa Ukawa na kurudi CCM, Ray Kigosi alisema walipokwenda Ukawa walidhani wanakwenda kwenye safari ya matumaini lakini baadaye waligundua haikuwa hivyo.
“Nimezunguka na Lowassa baadhi ya maeneo, lakini sijaona sera za maana na zenye mashiko. Ninawaambia vijana wenzangu mimi nimeshtuka na nyie hebu shtukeni,” alisema Kigosi.

Naye msanii wa filamu za Bongo Movie, Aunt Ezekiel aliwataka vijana kufanya kazi kwa kuwa hakuna mtu anayeweza kuwapa maendeleo, isipokuwa wenyewe.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini