Messi nje kwa majuma 8
Image copyrightReutersImage captionMessi nje kwa majuma 8
Mshambulizi hodari zaidi duniani Lionel Messi wa Barcelona hatashiriki mashindano yeyote kwa majuma 8 yajayo kufuatia jeraha la goti.
Mshambulizi huyo wa Argentina aliumia katika mechi ya ligi kuu ya Uhispania dhidi ya Las Palmas.
Barcelona ilishinda mechi hiyo mabao 2-1.
Messi mwenye umri wa miaka 28 aliondolewa uwanjani na kukimbizwa hospitalini kunako dakika ya 3 ya mechi hiyo.
Hata hivyo huenda mshindi huyo wa tuzo la mchezaji bora duniani akarejea katika mechi ngumu baina ya Barcelona na wapinzani wao wa jadi Real Madrid tarehe 22 Novemba.
Kocha Luis Enrique alisema kuwa atajitahidi kuendeleza mfumo wa mchezo wao hata bila ya messi kuwepo.
''Kutokuwepo kwa messi ni pigo ila tutalazimika kujifunga kibwebwe, na hili ninamaanisha kila mchezaji wetu atajikaza kisabuni ilikuziba pengo hilo japo ni kubwa...''Image copyrightAPImage captionRonaldo amecheza mechi 3 bila ya kufunga bao lolote
''Unajua vyema kuwa messi si mchezaji wa kawaida, mara nyingi amekwamua safu za ulinzi za timu nyingi wakati ambao hata mimi mwenyewe nahisi nimejitolea mzima mzima.'' Alisema Kocha Luis Enrique.
Licha ya kuondoka kwake mapema uwanjani, mshambulizi mwenza wa Barca,Luis Suarez alijifurukuta na kuwafungia mabingwa hao mabao mawili muhimu na kuisaidia kurejea kileleni mwa jedwali la la liga.
Real Madrid walijipata taabani pia baada ya kushindwa kufaidi uwanja wa nyumbani ,walipotoka sare tasa na Malagaat katika uga wa Bernabeu.
Villarreal kwa upande wao waliwazima mabingwa wa mwaka wa 2014 Atletico Madrid bao moja kwa nunge.