Ajali ya Noah yaua 5 huko Katavi

Watu watano wamefariki na wengine sita kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyokea kijiji cha Matandalani wilaya ya Mlele mkoani Katavi baada ya gari aina ya NOAH lenye namba T 451 DDP ikitokea Mpanda mjini Kuelekea Sitalike kupinduka na kuacha njia.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa tano za asubuhi baada ya gari kupasuka tairi na kupinduka ambapo chanzo cha ajali kikiwa mwendo kasi.
Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Mpanda Daktari Teopista Elista anasema walipokea majeruhi na miili ya marehemu majira ya saa sita mchana na kudai kuwa miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika hospital hiyo Majeruhi wa ajali hiyo wanaendelea na matatibabu na hali zao zinaendelea vizuri
Katika hali isiyokuwa ya kawaida Watoto wenye miezi tisa na miaka mitatu wamenusurika uku mama yao akipoteza maisha
Dereva wa gari hilo aliyejulikana kwa jina la Jastini Sizyindayasa anashikiliwa na polisi 
Katika hatua nyingine miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika chumba cha maiti hospitali ya Mpanda uku vifaa vya kuhifadhia Maiti vikiwa vimeharibika- See more at: http://edwinmoshi.blogspot.com/2015/09/ajali-ya-noah-yaua-5-huko-katavi.html#sthash.BgMTPaKg.dpuf

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini