Nuhu Mziwanda ni Limbukeni – BASATA
Baada ya Nuh Mziwanda kulitaka Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) kwenda na na wakati kuhusiana na jinsi inavyokwenda, baraza hilo limemjibu kwa kumuita limbukeni.
Akizungumza na na Planet Bongo ya EA Radio, Mkuu wa matukio wa baraza hilo, Maregesi alisema Nuh asidhani kufanya muziki wa nje ndio kuwa na soko.
“Huyo anayesema kitu kama hicho ana mawazo mfu,” alisema Maregesi. “Ninasema ana mawazo mfu kwa sababu ni limbukeni anataka kuiga kitu kisicho cha kwake kwa hiyo mi namwita limbukeni.”
Maregesi aliongeza kuwa kuiga muziki wa nje sio kupanua soko, isipokuwa ni ukosefu wa elimu ya sanaa.
“Asidhani kufanya muziki wa Marekani au wa Uingereza, au wa Nigeria ndio kuwa na soko, utakuwa na soko la wapi? Kwa sababu huwezi ukapiga muziki kuliko huyo mwenye chake. La tatu shida tuliyonayo ya wasanii wengi wa Tanzania tunafanya kazi ya sanaa bila kusomea.”
Maregesi amewataka wasanii kuthamini kazi za nyumbani na kujikita zaidi kufanya muziki wenye asili ya Tanzania kwani ndio utakaowapa soko LA kimataifa kwa utanzania wao.