FAIZA: Tuwe Tunahofu ya Mungu, Wanaomponda LOWASSA na WEMA

Saa nyingine ili uone uzito wajambo inabidi uvae viatu vya mwenzio- kwa kweli imefika wkt najisikia vibaya kuhusu kusoma ugonjwa wa LOWASA, watu wameona ndio fimbo ya kumchapia kuhusu ugonjwa wake kwa kweli sijisikii vizuri na sioni kama sawa

Pia katika pita pita huku insta nimeona Wema na mbwa na Zari na mtoto na maneno ya kashfa juu yake, jamani watanzania mnamatatizo gani kuhusu maisha ya watu!

Kwa nini unamsema vibaya mtu juu ya kilema chake ? Kwa nini usimsema mapungufu yake bila kumkashifu juu ya marazi au kilema ? Hii ni sawa kweli?
Nakumbuka kuna wakati watu walinisema sana kuhusu ukimwi! Nikawa najiuliza hii ingekua kweli na ukimwi ingekuaje ningejisikiaje tena kuna watu walikua wana nitukana live ikiwemo na kumwambia mtu ambae niko kwenye mahusiano nae, hivi mnazani kuna mtu ameomba marazi kweli.

Nyinyi mnaosema watu kuhusu vilema vyao je mnajua mnawaweka watu kwenye wakati gani?, hivi unajua kwa kumuandama mtu unaweza ukamuua au kumuongezea matatizo na saa nyingine kuchukua hatua mbaya.

Unae msema mtu unataka kuwa sababu ya matatizo yake ? Kama ni hapana basi tafazalini jamani tusemane yote lkn sio kwa mambo kama marazi au ugumba au kilema- jamani kabla hujafa hujaumbika tumuogope MUNGU tuwe tunahofu ya MUNGU
Faiza Ally @faiza_ally on Instagram

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini