CCM yasema iko tayari kupokea matokeo vituoni


Chama cha Mapinduzi Visiwani Zanzibar kimesema kimeridhia utaratibu wa tume wa kutangaza matokeo moja kwa moja kwenye vituo vya kupigia kura kwa kuwa kutajenga uwazi zaidi kwa wenye hofu ya kuibiwa kura.


Akizungumza kuhusu mwenendo wa kampeni visiwani humo Naibu Katibu mkuu wa Chama hicho Visiwani Zanzibar Bw. Vuai Ally Vuai amesema kuwa chama hicho hakina wasiwasi na utaratibu huo kwa kuwa kina uhakika wa ushindi.
Ameongeza kuwa pia utaratibu huo utakisaidia chama hicho pia kujua idadi ya kura walizozipatas katika ngome ya Wapinzani viwasani pemba ambayo itawajenga na kukiimarisha zaidi chama hicho.
Vuai ameongeza kuwa chama chake kimeiridhisha kushinda katika uchaguzi mkuu mwaka huu kuanzia ngazi ya madiwani hadi urais kwa sababu wananchi wameonesha kuwa na imani na chama hicho kwa kuwa kimetekeleza sehemu kubwa ya ahadi za mwaka 2010.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini